LICHA ya kuchangia asilimia 35 katika pato la taifa, bado
sekta isiyo rasmi haijapewa uzito unaostahili kwa kutoshiriki ipasavyo kwenye
hifadhi za jamii.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam na Mhadhiri wa Chuo Kikuu
cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Godbertha Kinyondo wakati wa uzinduzi
wa Mradi wa miaka minne utakaotafiti na kuonesha njia sahihi ya Sekta isiyo
rasmi kupata huduma za hifadhi za jamii.
“Tumeona tufanye utafiti ili kuona namna sahihi ya kusaidia
waliojiajiri kwenye sekta isiyorasmi kwa kuwa ni kundi kubwa linalofanya
biashara ndogondogo zinazochangia karibu asilimia 35 kwenye pato la taifa.
“Katika mradi huu tunaziangalia sekta za aina tatu zisizo
rasmi kwanza ujenzi, usafirishaji na wajasiriamali ambao ndio kundi kubwa… kama
bodaboda vijana wetu wengi wamejiajiri humu lakini hawana taarifa za kutosha
kuhusu haki yao ya kuingia kwenye hifadhi za jamii.
“Hawa mama lishe wengi lakini jiulize wangapi wamejisajili
na NSSF? Wangapi wanazo kadi za bima ya afya? Hawa madereva wa bodaboda kila
leo wanapata ajali wangapi wanazo bima za matibabu?.
“Hao ndio tunaowazungumzia na tumewaalika kwenye warsha hii
waje waseme changamoto zao na tutawaambia namna ya kutoka huko ili wafanye kazi
zao kwa furaha na amani wajue kwamba mchango wao kwa taifa ni mkubwa,” alisema
Dk. Kinyondo.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe (Utawala na Fedha), Prof. Ernest Kihanga, akisoma hotuba yake kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Miaka Minne utakaotafiti na kuonyesha njia sahihi ya sekta isiyo rasmi kupata Huduma za Hifadhi za Jamii.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.
Lone Riisgaard kutoka Chuo Kikuu cha Roskilde, akitoa mada.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...