Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatano Mei 16,2018 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi za Manispaa ya Shinyanga. Mkuu huyo wa wilaya amekabidhi vitambulisho 12,918 kwa maafisa watendaji wa kata 17 za manispaa hiyo watakaokwenda kugawa vitambulisho hivyo kwa wananchi. 

“Hapa nchini, hili ni zoezi la kwanza la ugawaji vitambulisho kwa wananchi kwa kutumia ugawaji wa mkupuo,tunaanzia katika manispaa ya Shinyanga,nakabidhi rasmi vitambulisho hivi kwa maafisa watendaji wa kata ambao watagawa vitambulisho kwa wananchi”,alieleza Matiro. 

Aidha aliwataka maafisa watendaji kuwa makini na kugawa vitambulisho hivyo haraka huku akisisitiza kuwa vitambulisho hivyo havitolewi kwa ubaguzi bali kila mwananchi ana haki ya kupata. 

“Zoezi kujiandikisha linaendelea katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga lakini kwa upande wa manispaa ya Shinyanga tumemaliza zoezi la uandikishaji kinachoendelea sasa ni kugawa vitambulisho,hili ni zoezi endelevu wale ambao hawajiandikisha wafike katika ofisi za NIDA kujiandikisha ili wapate vitambulisho”,aliongeza Matiro. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi la kugawa vitambulisho vya taifa (NIDA) kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Kushoto ni Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Agnes Machiya. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen Kapesa - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akiwasisitiza maafisa watendaji wa kata kuwa makini katika zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wananchi ili kuepuka changamoto inayoweza kujitokeza ya kupotea kwa vitambulisho.
Mratibu wa NIDA mkoa wa Shinyanga Nathanael Fredrick Njau akisoma taarifa ya zoezi la uandikishaji na utoaji vitambulisho vya taifa katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen Kapesa akizungumzia kuhusu zoezi la utoaji vitambulisho vya taifa.
Maafisa watendaji,madiwani na watumishi mbalimbali wa manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...