Na Emmanuel Masaka,Globu 

WATANZANIA watapata fursa ya kufanya malipo ya bima mbalimbali kwa njia rahisi zaidi kupitia simu zao za mikononi baada ya kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance na Maxcom kuingia makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara.

Akizungumza katika hafla ya utiaji sahihi makubaliano hayo jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman amesema sheria ya bima imebadilika, hivyo kuwataka wateja wa bima kufanya malipo yao  moja kwa moja kwenye kampuni za bima.

“Sheria ya bima huwa zinabadilika mara kwa mara kwa sasa sheria inamtaka mteja wa bima kufanya malipo bila kupitia kwa dalali au mawakala wa bima na tumegundua njia rahisi ya kuwawezesha wateja wetu ni hii ya kufanya malipo ni kupitia simu zao za mikononi,” ameongeza Suleiman.

Amesema utaratibu huo wa kulipa malipo ya bima kwa njia ya simu za mikononi unalenga kupanua wigo wa kulipa malipo na kuimarisha makusanyo ya michango na kumsaidia mteja wao kufanya malipo kwa njia rahisi zaidi ndani na nje ya nchini.

Amesisitiza kwa takwimu za hivi karibuni takribani asilimia 62 ya Watanzania wana miliki simu za mikononi ambapo ni sawa na watu milioni 20 lakini wanaofanya malipo ya bima  hawazidi laki moja.“Kwahiyo tumeamua kuungana na hawa ndugu zetu wa Maxcom ili kuwarahisishia wateja wetu kufanya malipo ya bima kwa njia ya simu za mkononi,"amesema Suleiman.

Hivyo amefafanua umuhimu wa kuingia kwenye malipo kwa njia ya simu kwa kuwa kwa mwaka watanzania wanaofanya malipo kwa njia ya simu za mkononi ni wengi na takribani Sh.bilioni 1.4 kwa mwaka miamala kwa njia ya simu hufanyika.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Maxcom, Jameson Kasati amefafanua mfumo wa kampuni yao wa kielectroniki ni imara na salama kwa wateja wa bima nchini kufanya malipo mbalimbali kama michango na kulipa ada kwa wakati wakiwa mahali popote.

“Tumejiunga na ulipaji wa njia ya kieletroniki na Serikali ambapo pia watu na kampuni binafsi wanaweza kupata fursa hiyo ya kufanya malipo yao kwa njia ya simu za mkononi katika juhudi za kuboresha ulipaji wa huduma mbalimbali nchini,” amesema  Kasati

Ameongeza uzinduzi wa huduma hiyo ni wakati muafaka wa watanzania kuweza kufanya malipo yao ya bima kwa njia ya simu za mkononi kwa mawakala mbalimbali ndani ya nchini. 
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman (wa pili kushoto), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa, Jameson Kasati, wakisaini  hati za makubaliano ya ushirikiano utakaowawezesha ulipaji rahisi wa bima mbalimbali kupitia simu za mkononi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine pichani ni maofisa wa Sanlam na wa Maxcom. 
Baadhi ya maofisa wa Maxcom  wakiwa  katika picha ya pamoja na viongozi wa Sanlam Life Insurance katika hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...