MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imeshauriwa kuanzisha klabu za mazingira katika shule zake za msingi za manispaa hiyo ili wanafunzi wafundishwe umuhimu wa utunzaji mazingira. 

Ushauri huo umetolewa Dar es Salaam jana na Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala Jabiri Makame wakati wa kampeni ya  upandaji miti shule msingi Yongwe iliyopo Chanika Ilala.

"Naomba Idara ya Mazingira manispaa ya Ilala muunde vilabu vya mazingira katika shule zenu za msingi ili wanafunzi wafundishwe umuhimu wa utunzaji wa mazingira"amesema Makame. Makame amesema suala la utunzaji wa mazingira ni letu sote hivyo inatakiwa tuweke mikakati mbalimbali jinsi ya uendelezaji na utunzaji wa mazingara. 

Afafanua ikiwekwa mikakati endelevu ya kuanzisha vilabu mashuleni wanafunzi wakafahamu jinsi  utunzaji mazingira serikali itakuwa imefaidika jamii nzima itapata elimu hiyo. Amewapongeza Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa juhudi zao kwa kuwekeza shule za msingi hasa upande wa mazingira na kuwataka wadau wengine Kushirikia na serikali. 

 Amesema utunzaji wa mazingira unafaida nyingi nchi yetu ikiwemo ya kuepuka jangwa,faida nyingine miti huleta kivuli na miti mingine ya matunda. Kwa upande wake Ofisa Elimu Msingi Ilala Elzabeth Thomas amesema Standard Chartered wameanza kampeni ya kusaidia shule za Msingi Ilala toka mwaka 2014  mpaka sasa wameweza kupanda miti 3300.

Amesema kuanzia mwaka 2014 hadi sasa wamekuwa wakishirikiana katika utunzaji wa mazingira  katika shule mbalimbali. Amesema awali kabla kupanda miti shule ya Yongwe kampeni hiyo ilianzia shule ya msingi Majani ya Chai, Pugu Kajiungeni, Buyuni, Kigogo Freshi, Viwege na Uhuru Mchanganyiko. 

Kwa upande wake Ofisa wa Benki hiyo  Isema Bilali amesema benki hiyo ilianza shughuli zake nchini mwaka 1917  na kwamba upandaji miti una faida nyingi ikiwemo kutuwezesha kupata mvua,ujenzi,inatupa chakula inazuia mmomonyoko wa udongo.  
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Yongwe Kata ya Chanika wakiwa katika wiki ya mazingira na upandaji miti shuleni kwao Dar es Salaam jana Picha na Heri Shaaban

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...