INSPEKTA Jenerali wa Polisi, Simon Sirro amewaonya watu waliopata msamaha wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa Aprili 26, 2018 wajichunge tabia na matendo yao.

Ametoa onyo hilo leo (Alhamisi, Mei 24, 2018) mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa vituo vya polisi vya kisasa vya Mburahati, Kiluvya-Gogoni na Mbweni ambavyo vimezinduliwa leo.

Alisema nia ya Mheshimiwa Rais Magufuli kuwapa msamaha ilikuwa njema lakini lakini kuna baadhi ya watu wameitumia vibaya fursa hiyo na hadi sasa watu watano wamekwishauawa na wananchi.

“Mheshimiwa Rais aliwapa msamaha baadhi ya watu mnamo tarehe 26 Aprili lakini wametumia vibaya msamaha na kurejea kwenye matendo yao maovu na hadi sasa watu watano wamekwishauawa na wananchi,” alisema.

Alisema anatoa onyo kwa wote waliopata msamaha na wana nia ya kurejea kwenye matendo yao maovu. “Ukitoka gerezani kwa msamaha, maana yake umerekebisha mwenendo wako na wananchi wanatarajia uwe hivyo, lakaini kama ukifanya vinginevyo, Serikali isilaumiwe,” alisema.

Akielezea kuhusu utendaji wa Jeshi la Polisi, Kamanda Sirro alisema tangu ashike madaraka hayo, jeshi hilo limewapeleka askari 1,267 kwenye mafunzo ya medani za kivita na kwamba jeshi hilo liko imara.

“Pia tumepeleaka askari wa upelelezi zaidi ya 1,000 kwenye mafunzo ya ujuzi na ustadi (skills and knowledge) wa kupeleleza kesi mbalimbali. Baada ya kuwapa mafunzo haya, tunataka kesi za kawaida upelelezi wake uwe umekamilika ndani ya miezi sita na zile kesi kubwa kubwa upelelezi wake uwe umekamilika ndani ya miezi 12. Tunataka kuhakikisha haki za Watanzania zinapatikana kwa wakati,” alisisitiza.

Kamanda Sirro alitumia fursa hiyo kumshukuru pia Rais Magufuli kwa kuwapatia sh. bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari; kutoa kibali cha ajira kwa askari wapya 1,500 na kuwaruhusu wawapandishe vyeo askari wenye kustahili kuanzia cheo cha Koplo hadi Naibu Kamishna wa Polisi (DCP).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...