KAMATI Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa  Zanzibar, leo tarehe 27 Mei, 2018 imefanya kikao chini ya  Mwenyekiti  wake ambae pia  Makamu Mwenyekiti wa  CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein. 

Dk. Shein amewataka  wajumbe wa Kamati Maalum ya NEC ya CCM Taifa Zanzibar kuendeleza kasi ya kuimarisha Chama kwa kutekeleza majukumu yao na kushuka kwa Viongozi na Wanachama wa ngazi mbali mbali ili CCM ishinde kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa  mwaka 2020.

Kauli hiyo ameitoa leo hii katika Kikao cha Kamati Maalum, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui Zanzibar. Pia kikao hicho kimepokea na kujadili taarifa za Viongozi Wakuu wa kitaifa, Wakuu wa Idara wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar pamoja na mikakati ya Chama kuelekea 2020.
Vile vile kikao hicho kimejadili mambo ya utendaji ya Chama Cha Mapinduzi ambayo yamepelekwa katika Vikao vya ngazi za juu kwa ajili ya kujadiliwa.Pamoja na hayo wajumbe wa Kamati hiyo wamepongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020  inayotekelezwa kwa ufanisi zaidi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kikao hicho ni cha  kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977 Toleo la 2017,Ibara ya 108(2).

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na:
CATHERINE PETER NAO
KATIBU WA KAMATI MAALUM YA NEC
ITIKADI NA UENEZI CCM-ZANZIBAR.
 Naibu  Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi akizungumza katika kikao hicho.
  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein(katikati) akiongoza Kikao Cha Kawaida cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Idd (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Abdulla Juma Saadalla (Mabodi).
 WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakifuatilia mambo mbali mbali katika kikao hicho.
WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakifuatilia mambo mbali mbali katika kikao hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...