Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella(aliyevaa kofia) akipokea vita nda  arobaini na magodoro yake kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Benki ya Exim Fredrick Kanga, wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure, kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa huo Rutachunzibwa Thoma.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, akiwashukuru na kuzungumza na wauguzi wa  Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure, wakati wa kukabidhi vitanda arobaini na magodoro yake kwa hospitali hiyo yaliyotolewa na Benki ya Exim.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Rutachunzibwa Thoma, akizungumza wakati wa kupokea vitanda arobaini na magodoro yake yaliyotolewa na Benki ya Exim kwa ajili ya Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Benki ya Exim Fredrick Kanga na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Stanley Kafu(kulia). 

BENKI ya Exim Tanzania leo imekabidhi vitandana magodoro 40 kwa Hospitali ya SekouToure ya mkoani Mwanza. 

Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka jana, kwa kuzindua mradi wa  mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujalijamii” ambao Benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania hasa kwenye kuboresha huduma za afya zinazotole wa kwa wakina mama na wanawake. 

Katika kukabiliana na uhaba huu unaosumbua taifa, benkiya Exim Tanzania, yenye uwepo wa kimataifa imeanzisha mradi unaolenga kusaidia upungufu wa vitanda katika wodi za wazazi kwenye hospitali nchini.

Hivyo benki ya Exim itatoa magodoro na vitanda 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini kamasehemu ya kampeni yake ya mwaka yenye lengo la kushirikiana na jamii.

 Mkuu wa mkoa wa Mwanza, JohnMongella alipongeza Exim Bank Tanzania kwa msaada wake na kuhimiza taasisi mbalimbali kutekeleza ishara ya Benkiya Exim Tanzania katika kusaidia kuboresha huduma ya afya hapa nchi.

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano, Mkuu wa idara ya rasilimali watu wa benki ya Exim, Bwana Frederick Kanga amesema, “Benki imetambua umuhimu wajumuiya zinazozunguka eneo la biashara yetu na ndio maana shughuli za kijamiini muhimu sana kwa Benkiya Exim. Tuna amini kwamba tuna sehemu kubwa katika kufanya mabadiliko mazuri katika sekta mbalimbali katika jamii zetu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...