Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepokea ujumbe wa wafanyabiashara wanne (4) kutoka Korea ya Kusini Mei 2, 2018 ukiongozwa na Rais wa Kampuni ya Gaon Cable Co. Ltd Jael In Yoon.

Kwa mujibu wa TIC ni kwamba Kampuni ya Gaon Cable Co. Ltd ni kongwe na imebobea katika utengenezaji wa nyaya za umeme mkubwa na wa kati huko Korea ya Kusini. Pia ni Kampuni hiyo mehusika katika kutengeneza miundombinu ya kusambaza umeme Korea ya Kusini kwa zaidi ya miaka 60.

Taarifa ya TIC kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam imesema ujio wa wafanyabiashara hao umefanyika kutokana na Kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini lililoandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania Korea ya Kusini na kufanyika Seoul Korea ya Kusini tarehe 31 Januari, 2018. 

Imeelezwa lengo la ziara hiyo ni kuangalia fursa za uwekezaji katika maendeleo ya sekta ya nishati hususani kufungua kiwanda cha kutengeneza nyaya nchini. Pia ujumbe huu umekuja ili kuonana na taasisi husika katika sekta ya nishati ili kufanya mazungumzo na kupata miongozo ya kuanzisha kiwanda hicho.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanya mkutano na wafanyabiashara hao na kuwapa taarifa zote muhimu. Kituo pia kimewahakikishia utayari wa kuwasidia katika hatua zote za uanzishaji mradi huo ikiwa ni pamoja na kuwapatia huduma mbalimbali kupitia mfumo wa Huduma za Mahala Pamoja. 

Huduma hizo ni pamoja na Usaidizi wa kupata ardhi kwa ajili ya uwekezaji, Kuandikisha Kampuni, Kujisajili na VAT, TIN, Kupata Leseni ya Biashara, Vivutio vya Uwekezaji, Kibali cha Kazi Daraja A na C, Hati za Ukazi daraja “A” na ‘’B”, Kusajiliwa kwa ajili ya kupata viwango vya ubora (TBS), Cheti cha uwezekaji, Kutathmini masuala yahusuyo mazingira (NEMC), Kusaidiwa kupata vibali vya usalama mahala pa kazi (OSHA) na Kusaidiwa upatikanaji wa vibali  kwa uwekezaji  unaohusisha chakula na dawa (TFDA).

Wakiwa nchini, wageni hao pia walifanya mikutano na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) kwa majadiliano na miongozo zaidi ya kuwekeza katika sekta ya umeme pamoja na kupata eneo la kuweka mradi huo. 

Imesisitizwa uanzishwaji wa kiwanda hicho nchini utakuwa na mchango mkubwa sio tu katika kukuza uchumi, kutengeneza ajira, kupunguza uagizaji wa nyaya bali pia kuimarisha njia za usambazaji wa umeme nchini pamoja na nchi jirani. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Mwambe (kushoto) akiwa  na Rais wa Kampuni ya Gaon Cable Jael Yoon baada ya kufanya mazungumzo kwenye ofisi za kituo hicho jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...