Na Mwandishi wetu.
VYOMBO vya habari nchini vimekumbushwa kwamba uhuru wa habari sio kuiangalia tu serikali, bali kujiangalia wenyewe na pia vyombo vyao vya habari.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe wakati akihutubia hadhira ya waandishi wa habari katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani, sherehe zilizofanyika kitaifa katika hoteli ya Morena Jijini Dodoma.
Katika hotuba yake baada ya kusikiliza hoja kadha kutoka taasisi mbalimbali kuhusiana na uhuru wa vyombo vya habari nchini na hisia kwamba vinaminywa Waziri huyo alisema kwamba ipo haja ya tasnia kujiangalia yenyewe kama inatenda haki na weledi kwa taifa hili.
“Kalamu ya mwanahabari ina nguvu sana, ina nguvu sawa na ya silaha, ikitumiwa vizuri ni mlinzi na ikitumiwa vibaya ni maafa” alisema Dk. Mwakyembe.
Alisema katika mazingira ya sasa ambako kuna walimu wengi kuna baadhi ya watu wanapiga kelele kuhusu kufuatwa kwa sheria wakisema sio demokrasia, huku wakifahamu fika kwamba hata katika nchi zao hicho wanachoimba demokrasia hakipo.Akihutubia kama mgeni rasmi alisema kwamba ingawa dirisha lipo wazi kwa majadiliano, serikali haitarudi nyuma kutokana na haja mahsusi ya udhibiti wa yanayoendelea katika mitandao kwa manufaa ya taifa hili leo na kesho.
“Kuhusu Kanuni za Maudhui Mtandaoni, hili tunaweza kukaa na kujadili lakini kama Serikali hatutarudi nyuma katika hili. “Kupitia mtandao, bila kuweka udhibiti kuna mambo mengi yanapita ambayo hatuwezi kukubaliana nayo” alisema Dk Mwakyembe.
Akiwasilisha salamu za Jukwaa la wahariri nchini TEF, Kaimu Mwenyekiti Deodatus Balile alisema kwamba ipo haja ya kuendesha mdahalo wa kitaifa kuhusu mustakabali wa uhuru wa habari nchini Tanzania ambao hatima yake ni amani na maridhiano.
Mgeni
rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison
Mwakyembe akizungumza kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku
ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena
jijini Dodoma.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya
Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du
Toit, akitoa salamu za Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Audrey Azoulay wakati wa kilele
cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Naibu
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Charles Stuart akitoa salamu za Umoja
huo wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Fausta Musokwa
akitoa salamu za TMF wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku
ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena
jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga akitoa salamu za taasisi hiyo wakati wa
kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Afisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Paul Mallimbo akitoa
salamu za Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kajubi Mukajanga wakati wa
kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Makamu
Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC),
Jane Mihanji akitoa salamu za UTPC wakati wa kilele cha sherehe za
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika
Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya
Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du
Toit akimkabidhi Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dk Harrison Mwakyembe nakala ya ripoti inayohusu uhuru wa
kujieleza na maendeleo ya vyombo vya habari wakati wa kilele cha sherehe
za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika
katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Katikati anayeshuhudia tukio hilo
ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika
(MISA-TAN), Salome Kitomari.
Mgeni
rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison
Mwakyembe akisalimiana na Mtaalamu wa Masuala ya Vyombo vya Habari na
Mkufunzi wa Kujitegemea, Rose Haji Mwalimu wakati wa kilele cha sherehe
za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika
katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mkuu
wa wilaya ya Kongwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Deogratius
Ndejembi akizungumza na washiriki wakati akifunga kilele cha sherehe za
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika
Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mgeni
rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison
Mwakyembe na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa
habari wakongwe (Veterans) mara baada ya kuhutubia kilele cha sherehe za
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika
Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...