· Kampuni hii inaleta furaha kubwa katika kituo cha kulelea watoto cha New LifeOrphans Home jijini Dar es salaam 

Dar es Salaam, Mei 26 2018 - QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja inayoongoza kwa kushirikiana na mwakilishi wake wa kijitegemea (IRs) kuleta shangwe na faraja kwa jamii mbalimbali zisizojiweza katika kuashiria mwezi mtukufu wa Ramadhan, katika nchi 13 za Kiafrika.

Kampeni hii ya mwaka ina lengo la kuboresha maisha ya wengi na inaenda sambamba na falsafa ya kampuni hii ya (RYTHM) Jiinue kuwasaidia wanadamu (Raise Yourself to Help Mankind) Mafunzo ya msingi ya (RYTHM) wakati wote yamekuwa yanalenga katika kuongeza juhudi zaidi ya wajibu katika kujali wale ambao hawana uwezo kwa kuwapatia mazingira mazuri ya kuishi kwaajili yao, hasa watoto ambao ni alama ya kizazi chetu kijacho.

Kampeni ya mwaka huu ya Ramadhan katika Afrika itashuhudia ushirikiano mkubwa miongoni mwa wafanyakazi wa QNET, wakala na Wawakilishi Binafsi (IR) wakiunganisha jitihada zao katika kuandaa mfululizo wa mwezi mzima wa shughuli za kutoa misaada katika nchi kama Ivory Coast, Togo, Cameroon, Guinea, Burkina Faso, Tanzania, Niger, Uganda, Chad, Mali, Ghana and Senegal.

Nchini Tanzania, tukio la utoaji wa misaada ya Ramadhan litashuhudia utoaji wa mchele, tambi, sukari na bidhaa zingine za chakula na matumizi kwa kituo cha Kulelea watoto yatima cha New Life Orphans Home jijini Dar es salaam yenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 9/-. 
 Meneja wa QNET, Muqtadir Suwani(kulia) akipeana mkono na Katibu wa  kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha New Life Orphans Home, Hamadi Kondo mara baada ya kutoa msaada wenye thamani ya zaidi ya milioni Tsh.9/- kwa kituo hicho kilichopo Boko jijini Dar es Salaam jana. 
 Meneja wa QNET, Muqtadir Suwani(wa tatu kutoka kushoto waliosimama nyuma) akiwa na mawakala huru wa kampuni ya QNET Tanzania mara baada ya kutoa msaada wenye thamani ya zaidi ya milioni Tsh.9/- kwa kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha New Life Orphans Home kilichopo Boko jijini Dar es Salaam jana.

 Meneja wa QNET, Muqtadir Suwani akizungumza na waandishi wa habari .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...