Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema watahiniwa 87,643 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita utakaoanza kesho Mei 7, 2018. Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde (pichani) amesema kuwa mtihani utahitimishwa Mei 25, 2018 ambapo amebainisha kwamba kati yao watahiniwa hao, wa shule ni 77,222 na wa kujitegemea ni 10,421.
Dk Msonde amesema mtihani utafanyika sambamba na wa kozi ya ualimu ambao watahiniwa 7,422 wa ngazi ya cheti na stashahada wamesajiliwa kuufanya.
"Maandalizi kwa ajili ya mitihani ya kidato cha sita na ualimu yamekamilika, ikiwamo kusambaza vijitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu mitihani hii," amesema Dk Msonde.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...