Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi  (CUF) Maalim Seif Shariff Hamad amewasilisha barua ya pongezi kwa katibu mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Dk. Bashiru Ally aliyeteuliwa kuongoza chama Hicho. 
Barua hiyo ya Maalim Seif ambayo imewasilishwa na msaadizi wake Bw. Mbaralala Maharagande saa chache baada ya kumalizika kwa  shamrashamra za kukabidhiana ofisi baina ya aliyekuwa katibu mkuu aliyestaafu  Ndg. Abdulrahman Kinana kwenye ofisi ndogo za CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo. 
 Maharagande amesema kuwa Maalim Seif ameandika barua ya hiyo ya pongezi mara tu baada ya Dr. Bashiru kuteuliwa kuwa katibu Mkuu mpya wa CCM. 
 “Katibu mkuu wa chama chetu ameandika barua kumpongeza Dr Bashiru na kumpongeza Katibu Mkuu aliyestaafu Ndg. Abdulrahman Kinana kwa kuweza kuimarisha demokrasia ya vyama kwa kipindi chote alichokuwa akiongoza CCM kwa kujali maslahi ya nchi kwanza kuliko mambo binafsi”amesema Maharagande. 
Amesema Dr Bashiru ni moja ya wasomi watakaoleta mabadiliko katika mfumo huu wa vyama vingi licha ya kuwa si vyema kutabiri atakachokifanya kwani watu wajue tu kuwa kiongozi huyu ni mzalendo ambaye anaamini katika mabadiliko makubwa katika masuala ya kisiasa. 
Bw. Mbaralala Maharagande, ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi  (CUF) Maalim Seif Shariff Hamad, akitoka kuwasilisha barua ya pongezi kwa katibu mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...