
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
MAKAMPUNI 380 yanayojishughulisha na Utalii yanataraji kushiriki Maonesho ya Kimataifa ya Karibu Kilifair huku kampuni ya Kilifair Ltd inayoratibu maonesho hayo ikitangaza kuandaa safari za kifamilia zitakazoshirikisha watu kutoka nchi mbalimbali Duniani kujionea vuvitio vya utalii kwa lengo la kuvitangaza kimataifa.
Maonesho ya kimataifa ya Utalii yaliyopewa jina la Karibu Kilifair yanafanyika kwa mwaka wan ne sasa yakiwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya Utalii wa Tanzania na nje ya nchi ,kwa lengo la kutangaza bidhaa mbalimbali za Utalii ikiwemo vivutio mbalimbali.
Kwa mara ya kwanza Kampuni ya Kilimanjaro SIR inayojishughulisha na ukoaji wa wageni waliopata matatizo katika maeneo yenye miinuko kama Mlima Kilimanjaro na Meru inataraji kushiriki katika maonesho hayo huku Shirika la ndege la Ethiopian Airlines likitangaza kutumia maonesho hayo kutangaza vivutio vya Utalii kwa wageni watakaosafiri na ndege wa shirika hilo.
Maonesho ya Karibu Kilifair yanayoratibiwa na Kampuni ya Kilifair Ltd awali yalijukiana kama Kilifair yakidhaminiwa na Kampuni mbalimbali za ndani na nje ya nchi .




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...