Malezi bora katika familia imesemeka ni ndio msingi wa malezi kwa watoto katika jamii yetu hivyo wazazi wanapaswa kuzingatia kutoa malezi bora kwa watoto ndani ya familia na jamii kwa ujumla ili kuwa na taifa lenye uchu wa kujiletea maendeleo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Vaileth Makota  wakati akisoma Hotuba ya Wziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika  maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.

Mhe. Vaileth Makota amesema kuwa wazazi wanawajibu wa kuwalea watoto katika malezi bora na katika maadili mazuri ili kujenga taifa bora lenye watoto wanaojitambua, wanaojithamini, na wenye maadili mema ili kulitumikia Taifa.

Ameongeza kuwa wazazi wanatakiwa kuwa walimu kwa matendo yao kwa watoto kwani watoto wanaiga yale ambayo wazazi wanafanya hivyo tabia na mienendo yao ni kati ya vitu ambavyo vitasababisha malezi mabaya au bora kwa watoto na jamii kwa ujumla.
 Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Vaileth Makota akiwasisitiza wazazi kuchangia ujenzi wa famila na taifa kwa kuwapa  malezi bora watoto  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mtoto Bibi Magreth Mussai akizungumzia umuhimu wa malezi bora katika familia na wajibu wa wazazi katika kutoa malezi hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Vaileth Makota( wa pili kushoto) akipokea bango la wadau kutoka nchi za ulaya wanaounga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania kupinga ndoa za utotoni wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.  
Nesi akimchoma mtoto wa Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Vanessa Makota Chanjo ya Saratani ya Shingo ya Kizazi katika uzinduzi wa chanjo hiyo Wilayani Kondoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani humo.  
Wanafunzi na Wananchi wa Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma wakifuatilia mambo mbalimbali katika Siku ya Familia Duniani yaliyokuwa yakifanyika katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...