-Mshindi kujinyakulia kitita cha Dola 50,000/-

 Kampuni ya TBL Group, chini ya kampuni  yake mama ya, ABIn Bev, Imewataka watanzania kuchangamkia kushiriki shindano lililozinduliwa  karibuni la wazo la ubunifu kupitia ujasiriamali, ,(The Africa Sustainability Challenge) linalolenga kukabiliana na changamoto zinazolikabili bara la Afrika na changamoto endelevu za kidunia.Ushiriki wa shindano ni kupitia tovuti ya www.challengeaccepted.africa

Washiriki  wa shindano ambao wazo la ubunifu  la ABinBev, litaibuka na ushindi watajishindia fedha za  kuwawezesha kutekeleza wazo lao kwa vitendo kiasi cha Dola za Kimarekani 50,000 (zaidi ya shilingi milioni za Tanzania.

 Akiongea juu ya shindano hili jijini Dar es Salaam,Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL Group,Irene Mutiganzi,alisema “Tukiwa kampuni kubwa ambayo ina mtandao wa kidunia tuna mtazamo wa kufanya uzalishaji wa vinywaji vya bia sambamba na kupitia vinywaji  hivi kuwaunganisha watu pamoja kwa miaka zaidi ya 100 ijayo,na lengo hili hili lifanikiwe tunahitaji mawazo shirikishi kutoka wadau mbalimbali nchini na barani Afrika kwa ujumla”.

Mutiganzi,alisema mawazo hayo ya ubunifu yanatakiwa kujikita jinsi ya kutatua matatizo yanayolikabili bara la Afrika ambayo baadhi yake ni kuhusu kilimo bora,changamoto ya maji,hali ya  hewa na  kukuza ujasiriamali endelevu.

 Shindano hili la mawazo ya kukabili changamoto la AB InBev Africa linawataka washiriki kutoka nchi mbalimbali kubuni jinsi ya kukabili changamoto zinazowakabili katika maeneo yao kama vile kukuza sekta ya kilimo,upatikanaji wa maji safi ,kuimarisha mifumo ya maji taka,kuwezesha familia zenye vipato vya chini,mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuongeza wigo wa ajira kwa watu wengi  katika jamii.

 “Hii ni fursa pekee kwa wajasiriamali wenye mawazo ya ubunifu wa kukabiliana na changamoto zilizobainishwa kuweza kujishindia safari ya kwenda Silicone Savannah jijini  Nairobi nchini Kenya sambamba na kujishindi dola za Marekani

50,000 za mtaji wa kuendeleza wazo lililoshinda  pia washiriki watapata fursa ya kushiriki katika mafunzo ya kuwajengea uwezo  na kushiriki katika mashindano ya ngazi ya dunia yatakayofanyika mjini Newyork nchini Marekani chini ya uratibu wa kampuni ya ABIn Bev”,alisisitiza.

Shindano hili liko wazi kwa washiriki kutoka nchi za Botswana, Ghana, Lesotho, Mozambique, Namibia, Nigeria, South Africa, Swaziland, Tanzania, Uganda na Zambia na mwisho wa kutuma  ni mwisho wa mwezi huu .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...