Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameutaka uongozi wa wilaya ya Gairo unamsimamia mkandarasi na kuhakikisha upanuzi wa kituo cha afya na unakwisha kwa wakati.
Akizungumza na uongozi na mkandarasi wakati wa ziara yake mwishoni mwa wiki iliyopita ya kukagua maendeleo ya Wilaya ya Gairo, Mhe. Kebwe amesema kuwa hajaridhishwa na kasi wanayokwenda nayo katika upanuzi wa kituo cha afya unaofanyika hivi sasa licha ya kuwa fedha za kituo hizo zote zimeshatolewa.
"Ni nini kinakwamisha ujenzi kuisha wakati fedha mmeshapewa???? amemuuliza Mkandarasi na Uongozi unaosimamia jengo hilo ... nawaomba sana, hebu fanyeni haraka maana kuna baadhi ya huduma wananchi wanakwenda kuzipatia mbali," amesema.
Amesema kuwa ipo haja ya kila mtu kutimiza majukumu yake bila ya kusukumwa sukumwa maana hali ya sasa ni kazi tu.
Awali akitoa maelezo ya ujenzi, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba amesema kuwa ujenzi huo umeshagharimu zaidi ya milioni 139 na baada ya kukamilika jumla ya wananchi wapatao 218,000 wataweza kupatiwa huduma huku vipimo vyote vikipatikana.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (aliyeshika tofali na
mwiko) na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi
nyekundu) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Rachel
Nyangasi (wa kwanza kulia) wakishirikiana kujenga ukuta wa Kituo cha
Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua
miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Mkuu
wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (aliyebeba tofali) kumsaidia
fundi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe
kujenga ukuta wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo
wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo
aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akikagua ujenzi kwa ajili
ya kupanua eneo la kulaza, na sehemu ya kuhifadhia maiti wakati wa ziara
yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akishiriki katika ujenzi
wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara
yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya
Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakimsikiliza Mganga
Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba (wa kwanza
kulia) wakati akitoa maelezo juu ya upanuzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya
cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...