Mkazi wa visiwani Zanzibar, Bi. Patricia Philipo amejishindia vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka Jumia kupitia kampeni iliyokuwa ikiendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ katika mwezi uliopita wa Aprili.
Mshindi huyo alipatikana kupitia kampeni iliyoendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. Wateja walitakiwa kupendekeza mtu wao wa karibu ambaye waliona anastahili nyumba yake kupendezeshwa na Jumia kwa kupatiwa ofa ya vyombo vya ndani.
Bi. Patricia Philipo aliibuka mshindi baada ya mchumba wake Bw. Mwalim Juma Kumpendekeza ashinde zawadi ya vyombo hivyo ili kumrahishia asije kusumbuka kununua tena pindi watakapofunga ndoa.
“Mimi ni mteja mzuri wa Jumia kwa sababu naitumia mara kwa mara kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali ambazo zimekuwa zikinifika mpaka ninakoishi Zanzibar. Baada ya kuliona hili shindano, niliona ni vema nimpendekeze mwenzangu ashinde. Ukizingatia tupo kwenye maandalizi ya ndoa yetu, suala la mahari pamoja na vyombo vya ndani ni gharama hivyo ushindi wake ungekuwa na mchango mkubwa kwenye shughuli yetu,” alisema Bw. Juma ambaye ni mchumba wa mshindi wa kampeni hiyo, Bi. Patricia.
“Sikuwa na wasiwasi kwamba endapo angeshinda asingeweza kupatiwa zawadi zake. Kwa sababu hapo nyuma kulikuwa na mashindano kadhaa kama vile ‘Treasure Hunt’ kipindi cha Mobile Week, wateja walikuwa wanashinda simu na kukabidhiwa bila ya ubabaishaji wowote,” alimalizia Bw. Juma.
Akielezea furaha yake mara baada ya kutangazwa mshindi Bi. Patricia Philipo amesema kuwa, “kusema ukweli hapo mwanzo sikutarajia kama ningeweza kushinda kutokana na ushindani mkali kutoka kwa mpinzani wangu. Kuna wakati nilitaka kukata tamaa kwa sababu mwenzangu alikuwa ameniacha mbali, mashabiki wake walikuwa wanamuunga mkono na kuwashirikisha wengine kwa kiasi kikubwa.”

Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni moja,Mkazi wa visiwani Zanzibar, Bi. Patricia Philipo mara baada ya kujishindia vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka Jumia kupitia kampeni iliyokuwa ikiendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ katika mwezi uliopita wa Aprili.
Bi. Patricia Philipo aliibuka mshindi baada ya mchumba wake Bw. Mwalim Juma Kumpendekeza ashinde zawadi ya vyombo hivyo ili kumrahishia asije kusumbuka kununua tena pindi watakapofunga ndoa. 

Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey akizungumza mapema leo jijini Dar kuhusu ushindi wa Mkazi wa visiwani Zanzibar, Bi. Patricia Philipo (hayupo pichani) aliyejishindia vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka Jumia kupitia kampeni iliyokuwa ikiendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ katika mwezi uliopita wa Aprili.Pichani kushoto ni Mchumba wa mshindi,Bw. Mwalim Juma.
Mshindi huyo alipatikana kupitia kampeni iliyoendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. Wateja walitakiwa kupendekeza mtu wao wa karibu ambaye waliona anastahili nyumba yake kupendezeshwa na Jumia kwa kupatiwa ofa ya vyombo vya ndani.
Afisa Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Hadija Natalia Tuwano pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey wakimsikiliza kwa makini Mchumba wa mshindi,Bw. Mwalim Juma akitoa ushuhuda wa namna alivyompendekeza Mchumba wake na kujishindia vyombo vya ndani mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,Mwalimu Juma alimpendekeza mchumba wake Bi. Patricia Philipo ashinde zawadi ya vyombo hivyo ili kumrahishia asije kusumbuka kununua tena pindi watakapofunga ndoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...