Na,Jumbe Ismailly, Singida
ASASI isiyokuwa ya kiserikali inayojishughulisha na utoaji elimu kwa njia ya kuburudisha kwa vijana waliopo katika shule za sekondari na walio nje ya shule ya FEMINA  imesema kwamba kupitia mpango wa nguvu ya binti umefanikiwa kupunguza kwa asilimia 70 utoro pamoja na mimba za utotoni katika shule za sekondari zilizopo katika mradi huo katika kipindi cha kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka huu.
Afisa Ufuatiliaji,Tathimini na Ufundi wa Femina,Marther Samweli Makala aliyasema hayo alipokuwa akiwasilisha mada kwenye mafunzo kwa vijana waliopo kwenye mpango huo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Romani Katholiki,mjini Singida.
Alifafanua Makala kuwa lengo la mpango huo ni kutoa elimu kwa vijana wa shule za sekondari wenye umri wa miaka kati ya 13 hadi 18 na walio nje ya mfumo wa shule walio na umri wa miaka kati ya 13 hadi 30.
Kwa mujibu wa afisa huyo tangu kuanza kwa FEMINA HIP hivi sasa ni miaka 19 na mwakani unafikisha miaka 20 tangu shirika hilo lilipoanzishwa na kila mwaka wanawafikia takribani watu milioni 15 wenye umri wa kati ya miaka 13 hadi 30 kupitia majaridi,redio,televisheni,facebook,tweeter, instagram pamoja na utube.
“Sisi kama shirika tumekuwa na mradi unaoitwa “Nguvu ya Binti” ambao umekuwa ukitoa elimu kwa wanafunzi waliopo mashuleni ya namna ya kujiepusha na utoro lakini pia kujizuia wasipate mimba za utotoni ambazo zinasababishwa na mambo mengi.”alisisitiza Makala.
Hata hivyo Makala aliweka bayana kwamba inaonekana kuwa kadri mrsi huo unavyoendelea kutekelezwa mimba za utotoni zinaendelea kupungua kwenye maeneo ambayo mradi umeanza kutekelezwa,lakini pia utoro kwa asilimia sabini umepungua.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Walimu walezi wa FEMA CLUB Taifa,Christopher Mavunde alisema kuwa hali ya mwanzo kabla ya mradi huo kulikuwa na mkanganyiko,kwani walikuwa wanapiga kelele juu ya athari za ndoa na mimba za utotoni,afya ya uzazi pamoja na madawa ya kulevya.


Walimu wa shule za sekondari zilizopo katika Mkoa wa Singida zilizopo katika mradi wa FEMINA HIP wakiwa katika mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na mradi huo katika ukumbi wa mikutano wa Romani Katoliki,mjini Singida.(Picha Na.Jumbe Ismailly)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...