Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Kangi Lugola ametoa muda wa miezi sita kwa kiwanda cha HUACHENG
kinachojihusisha na uchinjaji na usafirishaji wa nyama ya Punda Mkoni
Dodoma kuondoa mabaki ya miundo mbinu ya vyuma na mbao ambavyo
awali vilikua vikitumika katika uchinjaji wa ngo'mbe.
Mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika kiwanda hicho iliyolenga
kufuatilia maagizo ya Serikali yaliyotolewa hapo awali, Waziri Lugola
ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kutafuta wawekezaji ambao
wanaweza kutumia miundo mbinu hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya
Mifugo na Uvuvi. "Mvua itakaponyesha mahali hapa patakuwa na uchafuzi
wa hewa, na kwetu sisi wana mazingira magofu kama haya ni uchafuzi wa
mazingira, hivyo ndani ya miezi sita kama hamjapata ufumbuzi, ondoweni
mabaki haya". Lugola alisisitiza.
Aidha, Kiwanda hicho kimetakiwa kufuata takwa la kisheria la kufanya
Ukaguzi wa Mazingira kwakuwa awali kiwanda hicho kimekua kikifanya
shughuli zake bila kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira. Waziri Lugola
ameupa uongozi wa Kiwanda hicho muda wa miezi miwili kukamilisha
takwa hilo kama lilivyoainishwa katika Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004.
Katika ukaguzi huo Waziri Lugola amegundua pia kiwanda hicho hakina
Mpango Endelevu kama Sheria inavyoelekeza, hivyo Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limeagizwa kufuatilia utekelezaji
wa agizo hilo ndani ya miezi miwili.
Msemaji wa Kiwanda hicho Bw.Michael Gao amesema kuwa maagizo hayo
yatatekelezwa kikamilifu na kwa muda uliotolewa.
Kiwanda hicho huchinja punda ishiriki kila siku na wanasafirishwa
kupelekwa katika Nchi za China na Vietnam.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola
mwishoni mwa wiki ameendelea na ziara ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya
Mazingira. Pichani akipata maelezo kutoka kwa Afisa Afya wa Jiji Bw. Carle Lyimo mara
baada ya kutembelea kiwanda cha kuchinja punda cha HUACHENG kinachomilikiwa na
raia wa China.
Mganga wa Mifugo Bw. Merjoly Mariki Msimamizi wa viwanda vya nyama Kanda ya Kati
akitoa maelezo ya kitaalamu kwa Naibu Waziri Mhe. Kangi Lugola mara baada ya
kukagua kiwanda cha kuchinja Punda eneo la Kizoto Jijini Dodoma kwa lengo la
kukagua mifumo ya udhibiti wa taka.
Mabaki ya miundo mbinu ambayo awali ilikua ikitumika katika kuchinja ngombe katika
kiwanda cha HUACHENG Jijini Dodma ikiwa imetelekezwa baada ya mwekezaji huyo
kutoitumia tena na kujishughulisha na uchinjaji wa punda.
Sehemu ya punda wakisubiri kuchinjwa, imeelezwa kuwa nyama ya punda hao ina soko
kubwa sana katika Nchi za China na Vietnam. Wastani wa punda ishiriki huchinjwa kila
siku katika Kiwanda hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...