MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) umesema watatumia maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Jijini Tanga kuwahamasisha wafanyabiashara kujiunga nao ili waweze kunifaika na huduma za matibabu pindi wanakuwa wakikumbana na magonjwa mbalimbali.
Hayo yalisemwa jana na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Sophia Kaku wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao kwenye ufunguzi wa maonyesho ya sita ya biashara ya kimataifa yanayofanyika eneo la Mwahako mjini hapa.
Alisema watakapojiunga nao wataweza kuwa na uhakika wa matibabu wakati wanapougua lakini pia itawawezesha kuepukana na kutumia fedha nyingi pindi wanapokuwa wakiugua zinazotokana na kupanda kwa gharama.
“Ndugu zangu maradhi yanakuja bila taarifa hivyo iwapo tutawekeza kujiunga na mpango wa Mfuko huu unaweza kufaidika na matibabu lakini pia utaepukana na gharama kubwa za matibabu utakazopaswa kulipia wakati unapokumbana na magonjwa mbalimbali “Alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...