………………
Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) imetoa mafunzo ya uandishi wa habari za kitakwimu kwa wanachama wa
chama cha waandishi wa habari Dodoma ili kuwaongezea uwezo wa uandishi
mzuri wa habari za kitakwimu.
Mafunzo hayo ya siku mbili
kuanzia tarehe 26 hadi 27 Mei, mwaka huu yanayofanyika katika ukumbi wa
Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) Jijini Dodoma yamefunguliwa na
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa
kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara hiyo.
Akifungua mafunzo hayo
Zamaradi Kawawa amesema kutokana na Wizara zote pamoja na baadhi ya
Taasisi kuhamia Dodoma, Dodoma imekuwa ndio kitovu cha shughuli za
Serikali kwa maana hiyo imekuwa chanzo kikuu cha habari zinazohusu
Serikaki nchini hivyo basi majukumu ya vyombo vya habari vilivyopo
mkoani Dodoma yameongezeka na yatazidi kuongezeka kadiri shughuli za
Kiserikali zinavyoongezeka.
“Hapana shaka yeyote kuwa
watumishi wote wa vyombo vya habari vilivyopo Dodoma wanahitaji mafunzo
kama haya kwa ajili ya kuimarisha weledi wao katika kuripoti matukio
mbalimbali yanayotokea mkoani humu,” amesema Zamaradi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa akifungua mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa akifungua mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akisisitiza kuhusu namna idadi ya watu inavyoongezeka au kupungua wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Omary Mdoka akiwasilisha mada kuhusu ongezeko la watu wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Oscar Mangula akiwasilisha mada kuhusu Sheria ya takwimu ya mwaka 2015 wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Mariam Kitembe akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi hapa nchini kwa kuzingatia utafiti uliofanyika mwaka 2016/2017 wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Said Ameir akitoa maelezo kuhusu mafunzo ya siku mbili ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...