Usajili
wa Vitambulisho vya Taifa mkoani Morogoro umeendelea kwa wananchi
kujitokeza kwa wingi kusajili pamoja na changamoto kubwa ya mvua ambayo
imeharibu miundombinu na kufanya baadhi ya maeneo kutofikika kwa
kirahisi.
Akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Sanganjelu Kata ya Madege wilayani humo Afisa
Usajili Wilaya ya Gairo Ndg. Godwill Mwamanga amewahimiza wananchi
wanaoshiri zoezi hilo kuwa makini wanapojaza taarifa zao kwa kuhakikisha
wanajaza taarifa sahihi naza kweli ili kuepukana na usumbufu hapo
baadae.
‘Nawasihi
sana muwe wakweli kwenye taarifa zinazohusu umri, makazi na uraia wenu
ili taarifa zitakazo kusanywa zikajenge mfumo madhubuti wa Utambuzi wa
Taifa wenye taarifa sahihi za watu” alisisitiza
Kwa
sasa zoezi la Usajili linaendelea katika Kata ya Madege na Lesha ambapo
Kata zingine za Msingisi, Rubeho, Chanjale, Iyogwe, Italagwe na Mkalama
zimekamilisha zoezi. Kata za Nongwe, Gairo, Chagongwe, Chakwale,
Kibedya, Idibo, Nongwe, Mandege, Chagongwe, Ukwamani, Magoweko na
Ngiloli zitaendelea na zoezi kwa kuzingatia ratiba ya usajili
iliyotangazwa na Mamlaka.
Mkoa
wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa 21 inayoendelea na zoezi la Usajili
na Utambuzi wa Watu lenye kulenga kuwapatia wananchi Vitambulisho vya
Taifa.

Wananchi wa Kata ya Madege wakikatiza barabara kubwa ya Taragwe iliyojaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha; kuelekea kwenye vituo vya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwenye Kijiji cha Sanganjelu wilani Gairo.
Wananchi wa kijiji cha Iyogwe wakisikiliza maelekezo ya utaratibu wa kusajiliwa kutoka kwa Msimamizi wa kituo ambaye hayupo pichani.
Ndg. Juma Ally mkazi wa Kata ya Iyogwe Wilaya ya Gairo – Morogoro akipigwa picha na kuchukuliwa alama zake za kibaiolojia wakati zoezi la Usajili likiendelea.
Wananchi wakazi wa kijiji cha Kilama wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wakisikiliza kwa makini majina yao yakisomwa kuelekea kwenye chumba cha Usajili ikihusisha hatua ya kupigwa picha, kuweka alama za vidole na saini kileketroniki kwa kutumia mashine maalumu za kukusanya taarifa.
Afisa Usajili Wilaya ya Gairo Ndg. Godwill Mwamanga akizungumza na wananchi wakati wa kukagua maendeleo ya shughuli za Usajili kwenye kijiji cha Ngayaki kata ya Leshata.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...