Na Ankal
Unapopiga
picha ya ndege inayotumia pangaboi ni muhimu kuhakikisha kwamba kasi ya shata
(shutter speed) ya kamera yako sio ya juu sana ama sivyo picha utayopata ni ya
pangaboi kuonekana hazitembei wakati ndege ipo hewani, jambo ambalo litaua
uhalisia wa picha.
Kwa
kawaida kugandisha kitendo (action) ni jambo jema lakini kwa ndege picha
itaonekana ya mgando na isiyo na afya. Yaani kama ndege ipo angani na pangaboi
zimeganda itaonekana picha isiyotimia. Tatizo kwa wapiga picha wengi hasa
wanaotumia simu, aghalabu wakati wa mchana kamera za simu huwa zinajitega
kwenye “automatic’ hivyo shata inakuwa kwenye kasi kubwa. Kwa luigha ingine ni
kwamba kasi ya shata ikiwa ndogo itaonesha mzunguko halisi wa pangaboi.
Hii imepigwa kwa kamera ya kawaida aina ya Canon EOS 5D Mark lll
Hii imepigwa kwa simu ya Iphone 7.
The second picture is on upside down. The plane was on approaching landing with slow speed or landed already. U trick us Michuzi.
ReplyDelete