Na Leandra Gabriel, Blobu ya jamii
RAIS Mteule wa Urusi Vladimir Putin wa Chama cha Independent ameapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo baada ya kushinda Uchaguzi uliofanyika mapema Machi 18 mwaka huu.
Rais Putin anapata muda wa kuhudumu kwa mihula 4 zaidi, na amehudumu kama kiongozi wa Serikali kwa takribani miaka 18.
Katika uchaguzi huo Putin aliibuka na ushindi mnono wa zaidi ya asilimia 77 akiwamwaga Pavel Grudinin wa Communist party na Vladmir Zhirinovsky wa chama cha LDPR.Putin (65) alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza Taifa hilo mwaka 2000.Ambapo alihudumu kwa mihula miwili na akachaguliwa kuwa waziri mkuu kwa muhula mmoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...