Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-GAIRO. 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameliagiza jeshi la Polisi Wilaya ya Gairo kuwatafuta na kuwakamata watu walioharibu miundo mbinu ya maji ikiwemo kuiba pampu ya maji ya Kijiji cha Italagwe katika Wilaya ya Gairo na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria.

 Dkt. Kebwe ametoa agizo mapema leo Mei 24 mwaka huu akiwa katika Kijiji cha Italagwe Kata ya Italagwe, wilayani humo wakati wa ziara yake ya siku tatu ya kutembelea na kuhimiza miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro. 

Amesema kuwa changamoto kubwa inayowakumba wananchi wa Wilaya ya Gairo ni pamoja na tatizo la maji, hapati majibu sahihi kuona pamoja na changamoto hiyo bado kuna watu wanaodiliki kufanya hujuma ya kuiba miundo mbinu ya maji na kuwasababishia wengine kukosa maji. "Nashangaa sana kuona pamoja na changamoto mliyonayo ya maji ila kuna watu bado wanahujumu miundo mbinu yenu jambo linakosesha majibu sahihi, walioiba Pampu hiyo ya maji hawajatoka nje ya kijiji cha Italagwe... naomba OCD ufanye msako wa nyumba kwa nyumba ili kubaini mwizi na pampu ipatikane mara moja," amesema.

“OCD Mkong’oto utembee kwenye kijiji hiki. Mkong’oto utembee pampu ipatikane. Kuna wengine watachukulia kisiasa siasa suala hili, hiyo ndiyo kazi ya Mbunge kuangalia kwamba tunachangamoto gani asaidiane na wananchi” alisema Dkt. Kebwe “wezi wapo hapa hapa kijijini. DC banana na Afisa Tarafa, Mtendaji wa Kata, Mtendaji wa Kijiji, fanyeni Mkutano wa hadhara pampu ipatikane” alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akipokea maelezo ya wizi wa pampu ya maji kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe katika Kijiji cha Italagwe Kata ya Italagwe ili kuweza kuwalejeshea wanachi maji. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-GAIRO. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amesema nashangaa kuona pamoja na changamoto mliyonayo ya maji ila kuna watu bado wanahujumu miundo mbinu yenu jambo linakosesha majibu sahihi, walioiba Pampu hiyo ya maji hawajatoka nje ya kijiji cha Italagwe... naomba OCD ufanye msako wa nyumba kwa nyumba ili kubaini mwizi na pampu ipatikane mara moja.
Kisima kilichoibiwa pampu. 
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakielekea kukagua mradi wa maji uliokuwa unasumbua. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...