Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo. 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameuagiza uongozi wa wilaya ya Gairo na mkoa wetu kwa ujumla kuhakikisha wanafunzi wa shule msingi mpaka sekondani wanapatiwa chakula mashuleni. Kauli hiyo ameitoa wishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa katika Ufunguzi wa madarasa ya shule ya sekondari Chagongwe katika ziara yake kwa siku ya tatu Wilayani Gairo kukagua miradi ya maendeleo.

 Ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Gairo kujiwekea mpango kazi ili kuwawezesha watoto wote kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari wanapatiwa chakula cha mchana na kuwawezesha waweze kufanya vizuri katika masomo yao. 

"Watoto wa shule za Morogoro kutokula chakula mashuleni ni aibu, sitaki kabisa kusikia hili suala watoto kunyimwa chakula, naomba Mwenyekiti wa Halmashauri ya Gairo, upitishe azimio kwenye baraza na shule ambayo hawatatoa chakula shuleni wachukuliwe hatua uongozi wa eneo hilo," amesema Dkt. Kebwe.

 "Mkoa wetu unaongozwa kwa uzalishaji wa chakula cha kutosha sasa inakuwaje watoto wetu tuwanyime chakula, tutakosa matokeo mazuri," amesema.Aidha amesema kuwa mtoto anatakiwa kula chakula mara mbili ya mtu mzima, unapomnyima chakula hata ukuaji wake unakuwa hafifu... "Ubongo unatakiwa kupata chakula gram 6 za grucose" Amesema kuwa kukosekana kwa chakula shuleni kumekuwa kukichangia matokeo mabaya kwa wanafunzi bila kujali ni shule ya msingi au sekondari.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akifungua majengo ya shule ya Chagongwe wakati wa ziaya yake ya kukagua miradi ya maendeleo. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa pili kushoto) wakipiga picha ya ukumbusho mara baada ya kumaliza ufunguzi wa majengo ya shule ya sekondari Chagongwe.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Chagongwe waliojitokeza kumpokea wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Gairo na vitongoji vyake.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akikagua vyoo vya hosteli ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nongwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...