Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
MKUU wa Kikosi cha KJ 824 Kanembwa wilayani Kakonko Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Amosi Mollo amewapongeza vijana wa oparesheni Melelani walio hitimu mafunzo ya awali ya Jeshi la Kujenga Taifa( Jkt ) kwa andiko walilolifanyia kazi la utengenezaji wa sabuni ambalo litapelekea kuanzishwa kiwanda cha utengenezaji wa sabuni kikosini hapo.
Akizungumza jana wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi kwa vijana 732 wanaojitolea yaliyofanyika kwa miezi mitano, Mollo amesema katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Awamu ya tano wameandaa mpango wa kuanzisha kiwanda cha sabuni za kufulia.
Pia sabuni za kuogea na kunawia mikono ilikuhakikisha falsafa waliyowafundisha vijana hao ya kujitegemea katika ujasiriamali kwa kuwa vijana hao wamemaliza mafunzo ya awali wataendelea kujifunza stadi za maisha wakiwa kambini hapo.
Amesema
anawapongeza vijana hao kwa kujitolea kuandaa andiko la utengenezaji wa
sabuni ambalo wameanza kulifanyia kazi na sasa linaingiza pato kwa
Jeshi la Kujenga Taifa ambapo ni matokeo mazuri ya kujifunza na kutumia
elimu walioipata ya ujasiriamali, uzalendo, kujituma na kujitegemea
inayotolewa kambini hapo kuhakikisha wanaondokana na falsafa ya kwamba
hakuna ajira jambo ambalo limekuwa wimbo kwa vijana wengi mitaani.
Amesema nje na utengenezaji wa sabuni kikosi hicho kinajihusisha na ukulima wa alizeti, mahindi, kahawa na ufugaji wa nyuki na uchakataji wa asali, ufugaji wa mifugo mbalimbali na utengenezaji wa mafuta ya kupikia ya Alizeti.Amesema lengo ikiwa ni kuwajenga vijana wanaoingia kambini hapo kwa ajili ya mafunzo kuanza kujifunza namna ya ujasiliamali na kujitegemea hata watakapo rudi uraiani wakawe mfano na fundisho kwa vijana wenzao .
Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuja kujifunza namna ya ujasiliamali kikosini hapo, na kuwataka vijana walio hitimu mafunzo hayo kutumia mafunzo hayo kulinda amani ya Nchi na kujishughulisha katika shughuli za maendeleo ili kuondokana na umasikini uliopo katika familia zao.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika sherehe hiyo Mkuu wa wilaya ya Kibondo Louis Bura aliwapongeza wakufunzi wa kikosi hicho kwa kazi kubwa walioifanya ya kuwanoa wahitimu hayo na kuwataka vijana kuyaishi yale mema yote waliojifunza pamoja na mafunzo waliyo yapata waendelee kuonesha nidhamu na utii watakapo endelea kuwepo kambini hapo.
Aidha alimuomba mkuu wa kikosi kuhakikisha anatafuta soko la kuuza bidhaa hizo ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wakurugenzi wa halmashauri kununua sabuni za kusafishia vyoo na kunawia mikono katika kambi hiyo ili kuuunga Mkono jitihada za vijana na jeshi la kujenga taifa.
"Ntoe
pongezi zangu za dhati kwa wakufunzi wote najua mnafanya kazi katika
mazingira magumu lakini kwa uzalendo mlionao mmehakikisha vijana wetu
wAnajifunza namna bora ya maisha ikiwa ni pamoja na ujasili, uzalendo wa
kujitoa kwa ajili ya Nchi yetu pamoja na ujasiliamali hii ndiyo falsafa
tuliyo achiwa na waasisi wetu", alisema Bura.
Akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi mmoja wa Wahitimu hao Deogratiusi Mgaya amesema mafunzo hayo yamewajenga kuwa wazalendo na walipoanza mafunzo hayo walianza vijana 739 baadhi ya hao walishindwa kumaliza mafunzo yao kwa sababu ya Kifo cha mwenzao mmoja na utoro wa baadhi na kupelekea idadi ya walio hitimu kuwa 732 ambao wamepata mafunzo hayo ya awali.
Hata hivyo amewaomba wazazi kuwahimiza watoto wao kuingia jeshi la kujenga taifa ili kuwafanya vijana kuwa wazalendo na kuepukana na vitendo viovu pamoja na kujijenga katika kutegemea kujiajiri wenyewe na bila kusubili mpaka Serikali itoe ajira kwao.
MKUU wa Kikosi cha KJ 824 Kanembwa wilayani Kakonko Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Amosi Mollo amewapongeza vijana wa oparesheni Melelani walio hitimu mafunzo ya awali ya Jeshi la Kujenga Taifa( Jkt ) kwa andiko walilolifanyia kazi la utengenezaji wa sabuni ambalo litapelekea kuanzishwa kiwanda cha utengenezaji wa sabuni kikosini hapo.
Akizungumza jana wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi kwa vijana 732 wanaojitolea yaliyofanyika kwa miezi mitano, Mollo amesema katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Awamu ya tano wameandaa mpango wa kuanzisha kiwanda cha sabuni za kufulia.
Pia sabuni za kuogea na kunawia mikono ilikuhakikisha falsafa waliyowafundisha vijana hao ya kujitegemea katika ujasiriamali kwa kuwa vijana hao wamemaliza mafunzo ya awali wataendelea kujifunza stadi za maisha wakiwa kambini hapo.

Amesema nje na utengenezaji wa sabuni kikosi hicho kinajihusisha na ukulima wa alizeti, mahindi, kahawa na ufugaji wa nyuki na uchakataji wa asali, ufugaji wa mifugo mbalimbali na utengenezaji wa mafuta ya kupikia ya Alizeti.Amesema lengo ikiwa ni kuwajenga vijana wanaoingia kambini hapo kwa ajili ya mafunzo kuanza kujifunza namna ya ujasiliamali na kujitegemea hata watakapo rudi uraiani wakawe mfano na fundisho kwa vijana wenzao .
Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuja kujifunza namna ya ujasiliamali kikosini hapo, na kuwataka vijana walio hitimu mafunzo hayo kutumia mafunzo hayo kulinda amani ya Nchi na kujishughulisha katika shughuli za maendeleo ili kuondokana na umasikini uliopo katika familia zao.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika sherehe hiyo Mkuu wa wilaya ya Kibondo Louis Bura aliwapongeza wakufunzi wa kikosi hicho kwa kazi kubwa walioifanya ya kuwanoa wahitimu hayo na kuwataka vijana kuyaishi yale mema yote waliojifunza pamoja na mafunzo waliyo yapata waendelee kuonesha nidhamu na utii watakapo endelea kuwepo kambini hapo.
Aidha alimuomba mkuu wa kikosi kuhakikisha anatafuta soko la kuuza bidhaa hizo ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wakurugenzi wa halmashauri kununua sabuni za kusafishia vyoo na kunawia mikono katika kambi hiyo ili kuuunga Mkono jitihada za vijana na jeshi la kujenga taifa.

Akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi mmoja wa Wahitimu hao Deogratiusi Mgaya amesema mafunzo hayo yamewajenga kuwa wazalendo na walipoanza mafunzo hayo walianza vijana 739 baadhi ya hao walishindwa kumaliza mafunzo yao kwa sababu ya Kifo cha mwenzao mmoja na utoro wa baadhi na kupelekea idadi ya walio hitimu kuwa 732 ambao wamepata mafunzo hayo ya awali.
Hata hivyo amewaomba wazazi kuwahimiza watoto wao kuingia jeshi la kujenga taifa ili kuwafanya vijana kuwa wazalendo na kuepukana na vitendo viovu pamoja na kujijenga katika kutegemea kujiajiri wenyewe na bila kusubili mpaka Serikali itoe ajira kwao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...