Waziri ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Augustine Mahiga amesema Wizara hiyo itasimamia ipasavyo na kuhakikisha kwamba nia ya Mahujaji wa Tanzania waliojiandikisha kwenda kutekeleza Ibara ya Hijja Nchini Saudi Arabia Mwaka huu inatimia.
Amesema Wizara yake inafuatilia hatua za mwisho katika kuona tatizo lililojitokeza kwa Baadhi ya Taasisi za Usafirishaji Mahujaji Upande wa Tanzania Bara kukabiliwa na madeni Nchini Saudi Arabia linapata ufumbuzi wa haraka kabla ya kumalizika kwa muda wa mwisho wa uthibitisho wa Mahujaji wa Mwaka huu.
Dr. Augustin Mahiga amesema hayo wakati alipofika katika Makazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Bara bara ya Haile Selassie Jijini Dar es salaam kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya Hijja yaliyoleta usumbufu kwa Mahujaji wa Tanzania.
Amesema atalazimika kuzungumza na Mufti  Mkuu wa Tanzania pamoja na Uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) ili kujua hatua walizofikia katika kuona Taasisi zinazosimamia Usafirisdhaji Mahujaji upande wa Bara wamemaliza matatizo yanayowakabili.
Balozi Mahiga alimthibitishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Uongozi wa Wizara yake utalazimika kutoa baraka kwa Mahujaji wanaosimamiwa na Taasisi za Zanzibar pekee iwapo zile za Tanzania bara mpaka hatua ya mwisho zitashindwa kumaliza changamoto zao.
Hatua ya Balozi Mahige imekuja kufuatia baadhi ya Taasisi za Usafirishaji Mahujaji za Tanzania Bara kushindwa kulipa Madeni na kupelekea Wizara inayosimamia masuala ya Mijja Nchini Saudi Arabia kutishia kuzuia Mahujaji wa Tanzania kuingia Nchini humo kwa Ibada ya Hijja Mwaka huu.
Akigusia Miradi ya Kiuchumi inayolenga kustawisha Maendeleo ya Tanzania Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Afrika Mashariki Balozi Mahige alisema ipo haja ya kufuatilia Miradi iliyopata Mikopo na Ufadhili wa Kimataifa ili kujua maendeleo yake.
Balozi Mahige aliitaja baadhi ya Miradi hiyo ni ni pamoja na ile ya  Ujenzi wa Gati ya Mpiga Duri Kisiwani Unguja na ile ya Gati ya Wete Kisiwani  Pemba ambayo imo ndani ya Mpango Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Naye kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alimpongeza Balozi Maige kwa hatua alizoamua kuzichukuwa katika kukabiliana na changamoto zilizojitokeza kwenye masuala ya Hijja.
Balozi Seif alisema Ibada ya Hijja ni miongoni mwa nguzo Tano wanazowajibika Waumini wa Dini ya Kiislamu wenye uwezo kuzitekeleza ambayo imo ndani ya Imani za Waumini jambo ambalo wasimamizi wa masuala hayo wanalazimika kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Akielezea furaha yake kutokana na uamuzi wa Tanzania kuweka nia ya kutaka kufungua Ubalozi wake Nchini Jamuhuri ya Cuba Balozi Seif  alisema hatua hiyo muhimu itaongeza chachu ya uhusiano wa Kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Cuba.
Balozi Seif alisema Cuba ni Taifa la kwanza lililoyatambua na kuyaunga mkono Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 imekuwa mshirika mkubwa kwa Tanzania hasa katika kusaidia Taaluma kwenye miradi iliyomo ndani ya Sekta za Kilimo, Afya na hata masuala ya Viwanda.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dr. Augustine Maiga kwenye Makaazi yake barabara ya Haile Selassie Jijini Dar es salaam. Habari na picha na OMPR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...