Sherekea Sanaa ni tamasha la kipekee linalosheherekea sanaa na tamaduni za
Tanzania kwa njia ya mziki, miondoko, michoro na mengineyo. Nafasi Art Space
inawaalika tarehe 2 Juni kuanzia saa 12.30 joini mpaka saa 5 usiku kwenye tamasha hili
linalofanyika kwa ushirkiano wa Nordic Week.
Siku hio, ndani ya ukumbi wa Nafasi Art Space, kutakuwa na maonyesho ya sanaa ya
“Silence (ukimya)” zilizoandaliwa na wasanii mbali mbali nchini. Na kwenye jukwaa
makundi ya “Muda Dance” na “Nantea Dance” yameandaa maonyesho yao ya
miondoko ya kisasa, yaani contemporary dance.
Aidha, kwaya maarufu kutoka Denmark inaojulikana kama Nordlys Choir wataburudisha
wahudhuria. Pia dada Grace Matata atakuwepo kuwafuharisha mashabiki wa miziki wa
kizazi kipya.
Hivyo kutakuwa na kitu kwa kila mmoja. Tamasha hili la SHEREKEA SANAA ni bure na
wote mnaalikwa.
Tuma Barua pepe info@nafasiartspace.org kujua zaidi.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...