*Kutumia lugha ya Kiswahili katika kuutangaza
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd yenye chapa ya StarTimes imetangaza rasmi kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi mwaka 2018 Mubashara kupitia king’amuzi chake. StarTimes imethibitisha kuonesha michuano hiyo leo katika hafla fupi iliyofanyika Terrace, Slipway Masaki jijini Dar es Salaam na kushirikisha waandishi wa Habari pamoja na wadau mbalimbali wa soka nchini.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo David Malisa amesema “Mwaka huu katika Kombe la Dunia la 21, StarTimes ni mrushaji rasmi wa michuano hiyo itakayoanza Juni 14 hadi Julai 15 nchini Urusi. Mechi zote 64 zitakazochezwa Urusi katika Kombe la Dunia zitarushwa moja kwa moja.
" Amefafanua mbali na kurusha tu michuano hiyo maarufu zaidi Duniani, StarTimes watarusha matangazo ya michezo yote katika lugha ya Kiswahili na hiyo ni katika jitihada za kuienzi na kuikuza lugha ya Kiswahili lugha ambayo ni maarufu zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Meneja masoko wa Kampuni ya Startimes, David Malisa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi 2018 kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwenye king'amuzi cha Startimes.
Mkuu wa Kitengo cha Maudhui ya Startimes, Zamarad Nzowa akizungumzia namna walivyojipanga wakishirikiana na wasanii mbalimbali wa hapa nchini kwenye msimu wa kombe la Dunia litakalochezwa nchini Urusi hasa kwenye vipindi mbalimbali vitakavyokuwa vinarushwa kupitia kwenye king'amuzi cha Startimes.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la utangazaji nchini Tanzania (TBC), Edna Rajab akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni mbalimbali waliofika katika uzinduzi wa kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi 2018 kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwenye king'amuzi cha Startimes.
Balozi wa Startimes Tanzania kwenye msimu wa Kombe la Dunia na Msanii wa Bongo Movies, Wema Sepetu akizungumzia namna walivyojipanga na wasanii wenzake wakati wa kipindi chote cha Kombe la dunia wakishirikiana na Startimes Tanzania.
Mchambuzi wa Michezo, Jeff Leya akizungumzia fulsa aliyoipata mara baada kuingia mkataba na Startimes kuchambua mpira kwenye kombe la dunia kupitia king'amuzi cha Startimes.
Mkurugenziwa Startimes Tanzania, Wang Xiaobo akipiga mpira golini
Viongozi wa Startimes wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wakati wa wa uzinduzi wa kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi 2018 kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwenye king'amuzi cha Startimes kwenye ukumbi wa Hotel ya Slip Way jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...