Habari Njema! Balozi wa Italia nchini Tanzania, kwa mara nyingine tena atakuwa wenyeji wa onesho hili la Swahili Fashion Week Pop Up shop litakalo fanyika tarehe 2 mwezi juni kuanzia saa sita mchana hadi kumi na mbili jioni, ni sehemu pekee utakayopata nguo na vito vya hali ya juu kutoka kwa wabunifu mashughuli watakao simamia uuzaaji wa bidhaa zao bora.
Onyesho hili la siku moja lenye lengo la kuonesha bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kwa mkono kutoka kwa wabunifu wa ndani na nje ya nchi pamoja na wasanii wa uchoraji kutoka sehemu tofauti nchini Tanzania watakuwepo nyumbani kwa balozi wa Italia eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Onesho hili la pop up shop linawapa nafasi wafanyabiashara na wajasiriamali kuuza bidhaa zao kwa jamii ya kidiplomasia na watu wengine tofauti, pia litawakutanisha na wabunifu wa nguo, wabunifu wa vito, watengeneza mapambo ya ndani, na wasanii wa uchoraji.
Waandaaji wa Onyesho hili wanawasihii wajasiriamali wa kitanzania wanaokuza bidhaa “zinazotengenezwa Tanzania” kuchukua nafasi hii kukuza mtandao wakibiashara na kuongeza wateja na kupata nafasi ya kushiriki kwenye maonesho ya Swahili Fashion Week Bazaar yatakayo fanyika mwezi Disemba mwaka huu. Onesho hili lina jumla ya washiriki 40, baadhi yao ni, Jamilla Vera Swai, MM Collection, Xarafa, Neste Fashion Africa, Kiwohede, Naledi Tanzania, Lulua Gems, Diana Quilt and Designs, ABLO, Yasmar Perfumes, Kekuune, Hucna designs, Zawadi Zanzibari na wengine wengi.
Onyesho la SFW Pop Up shop linawakaribisha watu wote wafike nyumbani kwa balozi wa Italia, oysterbay, jumamosi ya tarehe 2 mwezi juni, hakuna kiingilio , vinywaji vitakuwepo na utapata nafasi ya kununua bidhaa mbalimbali kutoka kwa waoneshaji.
Swahili Fashion Week Pop Up shop imeandaliwa na kampuni ya mawasiliano na uratibu matukio, 361 Degrees Africa kwa kushirikiana na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mh. Roberto Mengoni
Kwa taarifa Zaidi na jinsi ya kushiriki tembelea tovuti yetu
www.swahilifashionweek.com au piga simu 0769 696 633/0713 844 486
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...