Na Ali Issa, Maelezo Zanzibar
Makatibu Mahsusi wa Taasisi za Serikali na Watu Binafsi Wametakiwa Kufanya Kazi zao Kwa Kufuata Sheria na maadili ya kazi hiyo kama zinavyo waelekeza ili kuleta ufanisi katika kazi.
Hayo yamesemwa Katika Hoteli Ya Mansoon Shangani na Mwenyekiti wa chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) Zuhura Songambele Maganga wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kuhusu mkutano Mkuu wa sita wa Chama hicho utakao fanyika chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar kampasi ya Tunguu.
Amesema kumekuwa na malalamiko juu ya makatibu mahsusi kufanyakazi kinyume na maadili ya kazi zao hivyo mkutano huo mkuu utaoaza kesho utaelekeza majukumu ya makatibu mahsusi wanavyotakiwa kutekeleza kazi kwa kufuata maadili ya kazi zao na mamlaka anayoifanyia kazi.
Aidha alisema kuwa makatibu hao wataelekezwa kufanya wajubu wao kwa kuthamini utaifa wao kwa malengo ya kuweka mbele maslahi ya nchi katika utoaji huduma bora kwa jamii.
“lengo la chama chetu mwaka huu ni kukuza taaluma, kudumisha uwajibikaji na kuinuwa hadhi ya taaluma ya katibu muhsusi kitaifa kimataifa,na kusaidia kudumisha utoaji huduma bora katika jamii” alisisitiza mwenyikiti TAPSEA.
Mwenyekiti wa chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TPSEA) Zuhura Songambele Maganga akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Mazsons Shangani kuhusu kufanyika mkutano wa sita wa Chama hicho unaoanza tarehe 10.5.2018 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Kempasi ya Tunguu.
Mwakilishi wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania upande wa Zanzibar, Zainab Ibrahim akieleza kuimarika kwa chama hicho kwa upande wa Zanzibar katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Mazsons Shangani.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...