MENEJA
wa Bandari ya Tanga (TPA) Percival Salama amesema wanajivunia
kuboreshwa huduma zao kwa kiwango kikubwa ikiwemo uandaaji wa nyaraka
kwa kasi na usalama wa kutosha kwa wateja na hivyo kutumia muda mfupi
kutokana na taasisi zinazohusika kuwepo sehemu moja hivyo kuwawia rahisi
kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati mmoja.
Salama aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye
viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya kimataifa ya
sita ya biashara ambapo alisema kutokana na hali hiyo hakuna sehemu
ambayo mteja anaweza kupita akikwama bila wao kujua mara kila hatua
wanazokuwa wakipitia wanatambua mara moja.
Alisema kuwa sehemu ambazo mteja anaingia kwenye bandari hiyo anapata
taarifa moja kwa moja hiyo ikiwa wanakumbana na vikwazo vya namna yoyote
zikijitokeza inawawia rahisi kuweza kuona na kuvishughulia kwa muda
mfupi ili kuweza kuondoa usumbufu ambazo unaweza kuwakabili
wafanyabiashara.
“Kwa kweli huduma za bandari ya Tanga tumeziboresha kwa kiasi kikubwa
kutokana na kasi ya uandaaji wa nyaraka lakini hata usalama wa kutosha
kwa wateja ambao wamekuwa wakiitumia hali iliyofanya kutumia muda mfupi
kutokana na taasisi zinazohusika kuwepo sehemu moja hivyo kuwawia rahisi
kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati mmoja “Alisema.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kushoto akisisitiza jambo kwa Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya kufungua maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...