TTCL PESA, Kampuni tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation, ambao ni watoaji wa huduma za fedha mtandao inapenda kuwajulisha Wateja, Wadau na Umma kwa ujumla kwamba, imefanya mabadiliko ya Jina na Nembo zinazoitambulisha Kampuni hiyo.
TTCL PESA ilizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan tarehe 18 Julai 2017 ikiwa na lengo kuu la kuwapa Wananchi huduma za kiwango cha juu kabisa cha ubora na unafuu wa gharama za kutuma fedha, kupokea fedha, kulipia huduma na kufanya miamala mbalimbali kwa kutumia simu zao.
Mabadiliko haya yanakuja miezi 9 baada ya TTCL PESA kuanza huduma zake kwa Mafanikio makubwa. Hatua hii ni kuridhia ushauri wa Wateja na wadau wetu waliopendekeza kufanyika mabadiliko ya jina na Nembo ili kuongeza mvuto wa huduma, kukidhi mahitaji ya Soko na urahisi wa kuitambua huduma hii miongoni mwa huduma zinazotolewa na Taasisi nyingine.
Huduma za fedha Mtandao ni Sekta inayokua kwa kasi duniani kote. Hapa Nchini Tanzania, miamala inafanyika katika jamii kupitia njia hii na kusaidia sana katika kuokoa muda, kurahisisha manunuzi, kutoa ajira kwa Makundi mengi ya wananchi hasa Wanawake na Vijana, kuongeza Mapato ya Nchi kupitia tozo za kodi, kuongeza usalama wa fedha na kuepusha uwezekano wa vitendo vya kihalifu kama wizi na utapeli visiweze kutokea kwa urahisi.
Kampuni
ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), imebadili nembo na jina la iliyokuwa
TTCL Pesa na sasa kujulikana kama T Pesa baada ya Uzinduzi uliofanyika
jijini Dodoma leo. (Picha:Mroki Mroki-Daily News Digital)
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION), Waziri
Kindamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Nembo ya na jina lipya la
TTCL Pesa.
Mgeni
Rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilaino (Sekta ya
Mawasiliano), Atashasta Nditiye akiwa amezindua Nembo mpya ya T Pesa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...