Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem hivi karibuni alizindua kisima cha maji safi na salama nambari 63 katika Chuo cha Ufundi cha Yombo kwa wanafunzi walemavu kilichopo Jijini Dar es salaam.

Uzinduzi huo ambao ulishuhudiwa na mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Josephine Lyungi, Kaimu Mkuu wa Chuo, Bi. Maryam, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kiwalani, Emannuel pamoja na walimu na wanafunzi. 

Huu ni mwendelezo wa mradi ulioanzishwa na Ubalozi wa Kuwait unaofahamika kwa jina la “KISIMA CHA MAJI KATIKA KILA SHULE”. Katika hotuba fupi iliyotolewa na Balozi Najeem,  alisema kuwa uzinduzi wa kisima hicho ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa mnamo tarehe Novemba 30, 2017 Chuoni hapo wakati wa uzinduzi wa "Mpango kamili wa kuwasaidia walemavu nchini Tanzania" wenye thamani ya dola laki tano kutoka Serikali ya Kuwait akiwa pamoja na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) Mhe.  Jenista Mhagama ambaye alimuomba Balozi ajenge kisima kituoni hapo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo, Bi. Maryam ameushukuru Ubalozi wa Kuwait kwa kuwajengea kisima ambacho kitawasaidia wanafunzi katika kufua, kuoga na kufanya usafi madarasani, mabwenini na maeneo mengine ya Chuo

Pembezoni mwa uzinduzi wa kisima cha maji, Al-Najem alitembea sehemu ya kujifunzia ushoni chuoni hapo kwa wanafunzi wenye ulemavu ambapo Ubalozi uliwahi kuchangia vyarahani katika ziara yake ya kwanza, na mara hii aliahidi kukipatia chuo hicho vitambaa na vifaa vyengine vinavyohitajika katika ushoni.
 Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akishuhudia wanafunzi wa Chuo cha Ufundi cha Yombo, wakiteka maji katika kisima alichokizindua hivi karibuni.
 Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi cha Yombo wakiendela na mafunzo yao wakati, Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem alipowatembela.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...