Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amepokea mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya Sh.milioni tatu kutoka Shirika la Bima la Taifa kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati.
Akizungumza na Michuzi blog, Ulega ameeleza leo kuwa mifuko hiyo ya saruji itatumika itatumika katika ujenzi wa zahanati katika vijiji mbalimbali kama Kibamba, kazole, Yavayava na Mkanonge wilayani humo.
Ulega amesema kuwa kazi hiyo ni ya wote katika kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli na kuifikisha Tanzania mbele zaidi na kusisitiza ujenzi wa miundombinu hasa ya madarasa na zahanati unaendelea katika vijiji mbalimbali na hiyo ni katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za msingi.
Aidha Ulega amelishukuru shirika hilo kwa msaada huo wa kusaidia Wilaya ya Mkuranga kwa ujenzi wa shule na zahanati.
Kwa upande wa Meneja Masoko wa Shirika la bima la taifa Elisante Maleko ameeleza utoaji wa mifuko hiyo ya saruji ni kutokana na uhusiano mzuri baina yao, hivyo wakaona faida wanayopata kutoka kwa wananchi hao ambao ni wateja wazuri ni kushiriki katika ujenzi wa miundombinu ya madarasa na zahanati katika vijiji mbalimbali vya Mkuranga.
Mkurugenzi wa Shirika hilo tawi la Ubungo Segeja Mabulla amemshukuru mbunge na mkuu wa wilaya hiyo kwa kuwakutanisha na kutoa elimu ya kuwasaidia wananchi kuhusu masuala ya bima.Pia amewapongeza wakazi wa Wilaya hiyo kwa kuwa wateja wazuri wa bima za halmashauri na bima za maisha.

Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akipokea
mifuko 200 saruji kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la bima
la Taifa,Elisante Maleko yenye thamani ya shilingi milioni tatu kwa
ajili ya ujenzi wa miundombinu ya zahanati na madarasa leo mkoani Pwani.
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akipokea
kava la tairi la gari kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la
bima Taifa,Elisante Maleko leo mkoani Pwani.
Naibu
Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga Uvuvi,Abdallah Ulega
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...