Mashindano
ya Copa Umisseta ngazi ya mikoa yanaendelea ambapo yamezinduliwa mkoani
Singida, katika uwanja wa Namfua ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa
mkoa huo, Dk. Rehema Nchimbi, aliyemwakilisha Waziri wa TAMISEMI,
Seleman Jafo.
Hafla ya uzinduzi huo wa michezo hiyo ambayo inadhaminiwa na kampuni ya
Coca-Cola pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani
humo, wadau wa michezo, walimu na wanafunzi wa shule za sekondari ambao
walishiriki kucheza michezo mbalimbali.
Mkuu
wa mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi katika hotuba yake ya ufunguzi,aliishukuru
kampuni ya Coca-Cola kwa kutoa udhamini kwa michezo hiyo na amewaasa
washiriki ambao ni wanafunzi kuyatumia kuboresha afya na akili ili
kuepuka kushiriki katika matendo ya kihalifu kama matumizi ya madawa ya
kulevya na kutojihusisha na mapenzi kabla ya wakati.
Alisema
mashindano hayo ni jukwaa kubwa la kuibua na kuendeleza vipaji vya
michezo na Ushahidi wa suala hili upo kwa kuwa kuna wanamichezo wengi
wanaotokea mkoani Singida ambao vipaji vyao viliibuliwa na Umisseta
vilevile mkoa huo katika mashindano ya mwaka jana ulifanya vizuri katika
ngazi ya kitaifa kwa kushika nafasi ya tatu.
Kwa
upande wake, Meneja Mauzo wa bidhaa za Coca-Cola mkoani Singida, Joseph
Simplis ,amesema Coca-Cola imekuwa ikidhamini mashindano haya kwa
kipindi cha miaka 3 na lengo kubwa ni kuhakikisha inawashirikisha
wanafunzi wengi zaidi nchini sambamba na kuibua na kukuza vipaji vya
michezo.Aliwaasa wanafunzi wa Mtwara kuchangamkia fursa hii.
Katika kufanikisha michezo hii, kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikitoa
udhamini wa vifaa vya michezo ambapo imelenga kusambaza vifaa kwa shule
za sekondari 4,000.
Katika
uzinduzi huo alikabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni kwa
wawakilishi wa shule mbalimbali mkoani humo.
Uzinduzi wa Copa Umisseta mkoani Singida ni wa tano kufanyika baada ya
kufanyika katika mikoa ya Dodoma, Tanga, Mtwara na Zanzibar. Mashindano
hayo ngazi ya kitaifa yatafanyika mwezi Juni mwaka huu mkoani Mwanza.
Wawakilishi wa shule za sekondari wakipokea vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni ya Coca-Cola kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi
Mkuu wa mkoa wa singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akifurahia zawadi ya mpira wa kufanyia mazoezi wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akijiandaa kupiga penati wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo. Na Mwandishi Wetu- Singida.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...