MKUU wa mkoa Dodoma,Dk.Binilithi Mahenge amepiga marufuku waajiri wote kutoa ahadi hewa kwa wafanyakazi wanaotangazwa kuwa wafanyakazi bora na badala yake wafanyakazi hao wanatakiwa kupewa zawadi zao na vyeti kadri ilivyopangwa na halmashauri husika au mwajiri.

Mkuu huyo wa mkoa alisema imekuwa desturi waajiri wamekuwa wakitafuta sifa ya kutangaza dau kubwa au zawadi kubwa kwa wafanyakazi waliotangazwa kuwa bora lakini kinyume chake wafanyakazi hao wamekuwa wakiambulia vyeti huku pesa hawapewi na linakuwa deni sugu.

Dk.Mahenge alitoa kalipio hilo baada ya wafanyakazi bora wa jiji la Dodoma pamoja na wafanyakazi bora wa Wilaya ya Chemba kupewa vyeti tu huku wakiahidiwa kupewa fedha baadaye badala ya kupewa fedha muda huo huo.

Akizungumza na wafanyakazi wakati wa utoaji wa vyeti, zawadi mbalimbali pamoja na fedha taslimu kiongozi huyo wa mkoa aliagiza mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,Godwin Kunambi pamoja na uongozi wa halmashauri ya Chemba kuhakikisha wanawapatia fedha zao wale wote waliochaguliwa kuwa wafanyakazi bora na si vinginevyo.

Alisema imekuwa tabia ya halmashauri nyngi kutangaza wafanyakazi bora na kutangaza kuwapatia vyeti na fedha taslimu lakini hawafanyi hivyo matokeo yake wafanyakazi wamekuwa wakizurumiwa au kupewa hundi feki jambo ambalo alisema ni kuwakatisha tamaa wafanyakazi wanaojibidisha kufanya kazi kwa bidii.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkta Bilinith Mahenge akizungumza na wafanyakazi katika maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi zinazofanyika duniani kote kila Tarehe 1 ya mwezi wa 5 zilizofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo kitaifa mwaka huu zinafanyika mkoani Iringa
Sehemu ya wafanyakazi wa mkoani hapa wakifuatilia Hotuba ya mkuu wa mkoa hayupo piachani) kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi zenye kauli mbiu ya kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Leo picha na Mahmoud ahmad Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...