NA Estom Sanga - DAR ES SALAAM 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umefanikiwa kutekeleza miradi 14,051 yenye thamani ya shilingi bilioni 502 Tanzania Bara na Zanzibar tangu kuanzishwa kwake mwaka 1999/2000. 

Akitoa taarifa kwa ujumbe wa Maafisa wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Sweden-SIDA waliotemebelea ofisi za TASAF jijini Dar es salaam na kisha kutembelea eneo la Makangarawe,katika Wilaya ya Temeke,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga ametaja miradi iliyotekelezwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya Elimu, Afya,Maji, Barabara, Hifadhi ya Mazingira, Kilimo ,ufugaji n.k ambayo ilitekelezwa kwa mafanikio makubwa kwa kuwashirikisha wananchi kwenye maeneo yao. 

Bwana Mwamanga amesema kutokana na Mafanikio ya awamu ya I na II ya TASAF, Serikali iliamua kuanzisha awamu ya III ambayo kwa kiwango kikubwa inajielekeza katika kuzikwamua Kaya zinazokabiliwa na umaskini uliokithiri baada ya kugundua kuwa hazikuwa zinanufaika na huduma zilizokuwa zinapatikana kwenye maeneo yao kutokana na umaskini. 

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF ameuambia ujumbe huo kutoka SIDA kuwa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini umeanza kuonyesha mafanikio na Walengwa wameanza kuwekeza katika miradi ya kiuchumi na hivyo kujiongeza kipato chao hususani katika nyanja za kilimo,mifugo na ujenzi wa nyumba huku suala la elimu na afyakwa watoto wao likipewa kipaumbele. 

Amesema hadi sasa TASAF inahudumia takribani kaya MILIONI MOJA NA LAKI MOJA ambazo zimeendelea kupata ruzuku na huduma nyingine kama elimu ya ujasiliamali, hifadhi ya mazingira,lishe, huku mkazo pia ukielekezwa katika kuhamasisha walengwa kuunda vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana ili kukuza shughuli za kiuchumi kwenye maeneo yao. 

Ujumbe huo kutoka SIDA baada ya kupata taarifa pia ulipata fursa ya kuuliza maswali juu ya Utekelezaji wa shughuli za Mpango na kujibiwa na Viongozi wa TASAF na kisha kuelekea katika eneo la Makangarawe,katika wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam ambako ulikutana na baadhi ya vikundi vya Walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini na kujionea biadhaa mbalimbali zinazotengezwa na walengwa hao kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. 

Hata hivyo katika maelezo yao,Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini huko Makangarawe wameonyesha kukabiliwa na tatizo la upatikanaji wa soko la bidhaa wanazozitengeneza huku pia wakiomba kupatiwa eneo mahususi kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao kwa ufanikisi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga akiwa ameshika kikapu alichokinunua kutoka kwa Kikundi cha Walengwa wa TASAF,katika eneo la Makangarawe ,wilaya ya Temeke,Jijini Dar es salaam bidhaa wanazotengeneza kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga (aliyeshika kitabu) akiangalia bidhaa zilizotengenezwa na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika eneo la Makangarawe,wilayani Temeke,Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga akiwa ameshika kikapu alichokinunua kutoka kwa Kikundi cha Walengwa wa TASAF,katika eneo la Makangarawe ,wilaya ya Temeke,Jijini Dar es salaam bidhaa wanazotengeneza kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga (wapili kutoka kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka SIDA waliotembelea Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika eneo la Makangarawe,wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam kuona namna walengwa hao wanavyonufaika na huduma za Mpango huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...