Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
WANAWAKE 200 ambao ni wajasiriamali mkoani Kigoma wanataraja kupata mafunzo yatakayosaidia kuwaimarisha kiuchumi na lengo ni kuhakikisha wanapata maendeleo katika mkoa huo na Taifa kwa ujumla hasa kipindi hiki cha kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda.
Awali akifungua rasmi mafunzo hayo jana mkoani humo na yanatarajiwa kudumu kwa siku 10 katika halmashauri zote mkoani hapa Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kigoma Gaden Machunda ametoa msisitizo kwa akina mama kujikita katika ujenzi wa viwanda.
Aidha Machunda amewataka akina mama kuzingatia misingi ya ujasiriamali pamoja na kuwa na nidhamu na biashara wanazozifanya huku akiwataka wauzaji wa hoteli na migawa kuwa nadhifu ili kuwavutia wateja.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya AJ General Company
amesema lengo la mradi huo ni kuwawezesha wanawake na kusaidia
kutekeleza Ilani ya Serikali ya awamu ya 5 kuelekea ujenzi wa Tanzania
ya viwanda.Ambapo amesema wanawake watainuka kiuchumi kupitia mpango huu
na wanawake watapata mikopo isiyokuwa na masharti kama ilivyokuwa hapo
awali lakini pia kuwezesha bidhaa zinazozalishwa mkoani hapa kupata soko
nje ya nchi.
Katibu wa Umoja wa Wanawake mkoani Kigoma (UWT) Edina Kuguru amesema wao kama viongozi wa wanawake wamejipanga kuhakikisha wanawake wote mkoani hapa wanaondokana na mfumo wa kuwategemea wanaume.Amesema mikakati waliyonayo ni kutoa elimu ya ujasiriama na jinsi ya kutumia fedha wanazopewe zinatumika ipasavyo na kuwatafutia masoko kwani wana mipango ya kuanzisha viwanda vya mihogo kwa kuwa zao hilo linalimwa sana mkoani Kigoma.
Mmoja wa wajasiriamali wa Mkoa wa Kigoa Maisala Barakabise amesema wanawake wa mkoa huo wanajitahidi kufanya biashara kwa kutumia mitaji yao na wao ndio walezi wa familia na ni wathubutu.Hivyo wakiwezeshwa wanaweza zaidi na kuongeza wamekuwa wakiibua fursa nyingi.
Amesema
changamoto wanazokumbana nazo katika kutafuta kipato na kujiondoa
katika dimbwi la umasikini ni mitaji modogo.Mjasiriamali mwingine Sakina
Kabeza amesema wanawake wa Kigoma ni wachapakazi na wanajituma na
kufafanua kipindi cha nyuma fursa zilikuwa ni chache lakini kwa sasa
Awamu ya tano imejipanga kikamilifu kutoa fursa kwa wanawake wote.
"Na endapo wanawake wa Kigoma wakipatiwa elimu na mitaji wanaouwezo wa kufanya vitu vya tofauti na wanao uwezo wa kuchangamkia fursa kujikwamua kimaisha,"amesema.Aidha ameipongeza taasisi hiyo iliyojitokeza na kutoa elimu na mikopo kwa wanawake mkoani Kigoma.
WANAWAKE 200 ambao ni wajasiriamali mkoani Kigoma wanataraja kupata mafunzo yatakayosaidia kuwaimarisha kiuchumi na lengo ni kuhakikisha wanapata maendeleo katika mkoa huo na Taifa kwa ujumla hasa kipindi hiki cha kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda.
Awali akifungua rasmi mafunzo hayo jana mkoani humo na yanatarajiwa kudumu kwa siku 10 katika halmashauri zote mkoani hapa Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kigoma Gaden Machunda ametoa msisitizo kwa akina mama kujikita katika ujenzi wa viwanda.
Aidha Machunda amewataka akina mama kuzingatia misingi ya ujasiriamali pamoja na kuwa na nidhamu na biashara wanazozifanya huku akiwataka wauzaji wa hoteli na migawa kuwa nadhifu ili kuwavutia wateja.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya AJ General Company
amesema lengo la mradi huo ni kuwawezesha wanawake na kusaidia
kutekeleza Ilani ya Serikali ya awamu ya 5 kuelekea ujenzi wa Tanzania
ya viwanda.Ambapo amesema wanawake watainuka kiuchumi kupitia mpango huu
na wanawake watapata mikopo isiyokuwa na masharti kama ilivyokuwa hapo
awali lakini pia kuwezesha bidhaa zinazozalishwa mkoani hapa kupata soko
nje ya nchi.Katibu wa Umoja wa Wanawake mkoani Kigoma (UWT) Edina Kuguru amesema wao kama viongozi wa wanawake wamejipanga kuhakikisha wanawake wote mkoani hapa wanaondokana na mfumo wa kuwategemea wanaume.Amesema mikakati waliyonayo ni kutoa elimu ya ujasiriama na jinsi ya kutumia fedha wanazopewe zinatumika ipasavyo na kuwatafutia masoko kwani wana mipango ya kuanzisha viwanda vya mihogo kwa kuwa zao hilo linalimwa sana mkoani Kigoma.
Mmoja wa wajasiriamali wa Mkoa wa Kigoa Maisala Barakabise amesema wanawake wa mkoa huo wanajitahidi kufanya biashara kwa kutumia mitaji yao na wao ndio walezi wa familia na ni wathubutu.Hivyo wakiwezeshwa wanaweza zaidi na kuongeza wamekuwa wakiibua fursa nyingi.
Amesema
changamoto wanazokumbana nazo katika kutafuta kipato na kujiondoa
katika dimbwi la umasikini ni mitaji modogo.Mjasiriamali mwingine Sakina
Kabeza amesema wanawake wa Kigoma ni wachapakazi na wanajituma na
kufafanua kipindi cha nyuma fursa zilikuwa ni chache lakini kwa sasa
Awamu ya tano imejipanga kikamilifu kutoa fursa kwa wanawake wote."Na endapo wanawake wa Kigoma wakipatiwa elimu na mitaji wanaouwezo wa kufanya vitu vya tofauti na wanao uwezo wa kuchangamkia fursa kujikwamua kimaisha,"amesema.Aidha ameipongeza taasisi hiyo iliyojitokeza na kutoa elimu na mikopo kwa wanawake mkoani Kigoma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...