Wilaya ya Kisarawe huenda ikawa wilaya ya mfano hapa nchini kwa wananchi wake wote wenye ulemavu kupatiwa bima ya afya iliyoboreshwa. 

Neema hiyo kwa walemavu imetokea leo wakati wa zoezi la ugawaji wa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu vilivyo tolewa na shirikisho la watu wenye ulemavu nchini(SHIVYAWATA).

Katika hafla hiyo ya ugawaji vifaa saidizi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo ambaye pia ni mbunge wa wilaya hiyo ya Kisarawe ametangaza neema hiyo kwa walemavu hao kwa kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kisarawe kufanya utaratibu wa kupata Sh.milioni 6 kutoka mapato ya ndani ili kuwalipia CHF iliyo boreshwa kwa vikundi 207 vya walemavu.

Amesema lengo ni walemavu wote wa wilaya hiyo wawe na uhakika wa kupata huduma ya afya ambapo kwasasa wilaya ya Kisarawe ina jumla ya watu wenye ulemavu wapatao 1608. Waziri Jafo ametoa msisitizo kwamba kwa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe haiwezi kushindwa kupata sh.milioni 6 ili kuwalipia walemavu.

Baada ya maelekezo hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Mussa Gama amethibitisha Waziri Jafo kuwa watahakikisha wanatekeleza agizo hilo kabla mwezi Juni 2018. Katika hatua nyingine, Mkuu wa mkoa wa Pwani Eng. Ndikilo amemuagiza Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani Zuberi Samataba awaandikie wawekezaji wote wa viwanda wa mkoa wa Pwani waone namna watakavyoweza kuchangia vifaa saidizi cha walemavu ili walemavu wengine waliobaki waweze kusaidiwa vifaa hivyo wezeshi. 

Naye, Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mhe. Happiness Seneda ameitaka jamii kushirikiana ili kuwasaidia watu wenye ulemavu wilayani Kisarawe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Kisarawe.
baadhi ya watu wenye ulemavu waliokabidhiwa vifaa wezeshi.
Baskeli za watu wenye ulemavu walizokabidhiwa.
Baadhi ya wananchi wa Kisarawe walio hudhuria mkutano wa ugawaji wa vifaa wezeshi vya walemavu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...