PICHA NA HABARI Za Freddy Macha
 Jumuiya ya Wasanii Watanzania Uingereza (WASATU) ilichemsha supu, ukumbi wa Heartlands , Birmingham, Uingereza Jumamosi iliyopita. Makutano haya yalikuwa pia sehemu ya mchango mahususi kusaidia wasichana wanaopewa mimba kabla ya kuwa watu wazima, vijijini, Arusha. Fedha zilikusanywa na mjasiriamali mkazi wa Birmingham, Mtanzania Sia Travel. 
Sia alijaa mlangoni akihakikisha kila senti iiliyolipwa na wahudhuriaji watashiba chakula , sanaa usiku kucha na kuwafariji vigoli wetu, Tengeru. WASATU iliyoundwa mwaka 2016 chini ya udhamini wa Balozi, Uingereza, Mhe Asha Rose Migiro, inakutanisha wasanii wa ala mbalimbali chini ya viongozi- mwanamuziki na mcheza sarakasi mwenye nidhamu ya hali yajuu, Fab Moses na mtangaza mapishi ya Kitanzania, Uingereza, Bi Neema Kitilya, aliyetulizana kama shingo ya twiga....Mwaka jana, 2017, shughuli hii ilifanywa Northampton na asilimia 20 ya kipato iliwafikia Watanzania waliofikwa na maafa ya mafuriko ya maji.

3-bango la WASATU 
7- Ramasax akipuliza vituz- pic by F Macha 2018 
 Rama Sax akipuliza vitu. Zamani alipiga na Simba Wanyika akashiriki kurekodi wimbo wa “Sina Makosa”. Rama Sax pia ni mwimbaji mahiri
2- Warembo walioonesha mavazi ya Kitanzania- pic by F Macha 2018Warembo wa kujitolea, walioonesha mavazi yaliyoandaliwa na kampuni ya “All Things African” (inayoendeshwa na Mtanzania, mchapa kazi, asiyejua uvivu kabila gani, Hamida Mbaga). Toka kushoto, Yvonne Waweru, Georgeous Katega, Victoire Koleilas, Maureen Tibenda
13- Mwanamuziki Saidi Kanda akiwa na WatanzaniaMwanamuziki Saidi Kanda,(aliyesimama) mtukuzaji vyombo asilia vya muziki wa Kitanzania, akijumuika na Wabongo nadhif, waliokuwemo14- F Macha, ikiwa Ismail na Rama SaxMwandishi na mtunzi, Freddy  Macha pamoja na Likiwa Ismail (ngoma) na Rama Sax. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...