Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Azzan Mussa Zungu akiongoza kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.
 Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt Mary Mwanjelwa akieleza mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa zao la korosho  linaendea kuwanufaisha wakulima Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Rais wa Umoja wa Vijana wa Bunge la Afrika na Mbunge wa Handeni Vijijini Mhe.Mboni Mhita  wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.
 Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula akitolea ufafanuzi tofauti iliyopo kati ya shule za Serikali na Binafsi na kusisitiza kwamba mitaala ya kimataifa imeruhusiwa ili kukidhi mahitaji ya raia wa kigeni wanaoishi nchini.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt.Philip Mpango akizungumza jambo na Mbunge wa Bunda Mjini wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Jacqueline Ngonyani akiomba ufafanuzi kwa Serikali kuhusu ulipaji wa Mawakala wa pembejeo wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiwasalimie wabunge wakati wa utambulisho wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof Ibrahim Juma (kushoto)  wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.
Picha zote na Daudi Manongi, DODOMA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...