Na Agness Francis,Blogu ya Jamii
KIKOSI cha Timu ya Yanga SC kimeondoka leo kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya kucheza na Timu ya USM Alger Nchini Algeria katika hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.
Wawakishilishi hao wa Tanzania ambao wanatarajia kucheza na USM Alger katika mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi kombe la shirikisho wanaondoka leo saa 11 jioni kupitia Dubai.
Yanga wamesafiri na wachezaji 20 pamoja na viongozi 8 wakiwepo na benchi la ufundi ambapo mtanange huo utachezwa nchini Algeria Mei 6 mwaka huu saa 4 Usiku.
Akizungumza leo katika Makao makuu ya Yanga jijini Dar es Salaam, Msemaji wa kikosi hicho Dismas Ten amewataja baadhi ya wacheza ambao wapo katika msafara huo ni Rostand Youth,Ramadhani Kabwili,Gadiel Maiko,Obrey Chirwa,Pato Ngonyani,Kelvin Yondani,Ibrahim Ajibu. Dismas Ten amesema wachezaji hao ni wale ambao wapo katika programu ya mwalimu,
"Tunahitaji matokeo na maandalizi ya muhimu yameshafanyika ukizingatia tupo ugenini.Mchezo ni mgumu na kikosi cha USM Alger kipo vizuri, si timu ya kuibeza wapo kwenye michuano haya ya kimataifa kwa mudu mrefu,"amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...