WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote nchini washirikiane na wadau wa mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kuanzisha kampeni ya kuhamasisha wananchi hususani wanaume kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema.
Kadhalika, amewaagiza Wakuu hao wa Mikoa na Wilaya kwa kusaidiana na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wasimamie kwa uzito unaostahili kampeni hiyo itakayoendeshwa kwa muda wa miezi sita mfululizo.
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumanne, Juni 19, 2018) wakati akizindua kampeni ya Kitaifa ya kuhamasisha wananchi hususani wanaume kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema, iliyofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri, jijini Dodoma.
“Kwa vile tunazindua kampeni ya kupima na kuanza ARV mara moja (Test and Treat) natoa rai kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI, mhakikishe vitendanishi na dawa za ARV zipo za kutosheleza katika kila kituo kinachotoa huduma katika kila Mkoa na Wilaya,” amesema.
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwahamasisha watu wote watakaogundulika na maambukizo ya VVU waelewe kuwa utaratibu wa sasa ni kuanza dawa mara moja pasipo kujali kiwango cha kinga mwilini, yaani CD4.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wakati alipozindua Kampeni za
Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja vya
Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, akizindua Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU
na kuanza dawa mapema, uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipokea tuzo ya kutambua kukubali kuwa
Balozi wa kuhamasisha wanaume kupima VVU nchini, kwenye Uzinduzi wa
Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, uliofanyika
kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018, kutoka kushoto ni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Jenista Mhagama na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Afisa Muuguzi Msaidizi Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Flora Kamwela, wakati alipozindua Kampeni za
Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja wa
Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akihamasisha upimaji wa Virusi vya Ukimwi
hususani kwa wanaume, wakati alipozindua Kampeni za Kuhamasisha Upimaji
wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Juni 19, 2018, kulia ni Sajenti Deogratius Peter.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa maelezo na kapteni Geofrey Mwajombe
katika Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema,
kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018, katikati ni
Sajenti Deogratius Peter.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo, akihamasisha pimaji wa
VVU hususan kwa wanaume, wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Kuhamasisha
Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini
Dodoma Juni 19, 2018, kulia ni Sajenti Deogratius Peter.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...