Kampuni ya ASAS Dairies inapiga kambi katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayotarajia kuanza kesho Juni 28 mwaka huu katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ambapo maandalizi ya banda lao kwa ajli ya kuwahudumia wateja wao limekamilika.
Kwa sasa maziwa ya ASAS ndio yamekuwa yakipendwa kila kona ya nchi yetu na katika kuhakikisha wanawahudumia watanzania kokote walipo wameamua kuweka banda lao kwa kuhakikisha wanaendelea kuwahudumia wote watakaofika kwenye maonesho hayo.
ASAS kutokana na kutambua kuwa kwenye viwanja vya Sabasaba idadi ya watu itakuwa kubwa nao wameamua kuchukua banda lenye uwezo wa kuingiza watu ndani na uamuzi huo ni kuhakikisha wanamhudumia kila anayeingia katika banda hilo.
Mmoja waandaaji wa banda la ASAS ameiambia Michuzi Blog kuwa mwaka huu wameamua kuweka maeneo mengi ya kuhudumia wateja watakaofika huku wakihakikisha hali ya hewa muda wote inakuwa rafiki kwa wote.
Mkazi wa Mtoni kwa Aziz Alli jijii Dar es Salaam ambaye alifika kujionea maandalizi ya maonesho hayo Juma Shaban amesema kuwa maziwa ya Asas yamekuwa na ladha ya aina yake ambayo inasababisha watu wengi kuyanunua.
Hivyo anaamini idadi kubwa ya watu watakaokwenda kwenye maonesho hayo lazima watafka katika banda hilo kama si wakubwa basi watoto ambao wengi wao wanapenda maziwa ya ASAS.
Muonekano wa nje wa banda la ASAS



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...