Habari tulizozipata Globu ya Jamii  hivi punde kutoka mkoani Kigoma mapema leo asubuhi hii ya Jumatano Juni 6,2018, inaelezwa kuwa Basi la Hamida Trans lenye namba za usajili T 885 DLD lililokuwa likitoka Kigoma kwenda wilaya ya Nzega mkoani Tabora limegonga treni ya mizigo (Garimoshi la mizigo) katika eneo la Gungu Mjini Kigoma.

Ripota wetu Editha Karlo aliyekuwepo eneo la tukio na kushuhudia mandhari halisi ya jali hiyo,ameeleza kuwa ajali hiyo imetokea leo alfajiri, na mpaka sasa  kwa taarifa za awali inaelezwa kuwa Watu 11 wanahofiwa  kupoteza maisha,huku idadi ya majeruhi ikidaiwa kuwa ni 26.

Ripota wetu yupo eneo la tukio,hivyo tutaendelea kuwaleta habari kadiri ya zitakavyokuwa zikiingia.
 Baadhi ya majeruhi wa ajali wakiendelea na matibabu katika hospitali  ya mkoa wa kigoma.
 Baadhi ya vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa eneo la tukio la ajali
 Baadhi ya Askari wa JWTZ wakiwa tayari wamefika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada kwa namna moja ama nyingine
 Baadhi ya Wananchi waliofika kushuhudia tukio la ajali hiyo wakishuhudia majeruhi wakipakizwa kwenye gari  ya Wagonjwa ya JWTZ tayari kupewa huduma ya kwanza na baadae kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi
Mbunge wa Kigoma mjini Mhe.Zitto Kabwe akiwa eneo la tukio la ajali akishuhudia majeruhi wakiokolewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...