Video
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana, alipotembelea
kijiji hicho kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba
Swagaswaga.
Na Hamza Temba-WMU-Chemba, Dodoma
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa siku 30 kwa wananchi
waliovamia Pori la Akiba Swagaswaga na kuendesha shughuli zao ikiwemo kilimo,
makazi na ufugaji ndani ya pori hilo kinyume cha Sheria waondoke mara moja kwa hiari yao kabla ya
kuondolewa kwa nguvu.
Ametoa
agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Handa Wilaya ya
Chemba mkoani Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua mgogoro wa ardhi
kwenye hifadhi hiyo wilayani humo.
"Tunawapa
siku 30 muanze kutoka wenyewe, baada ya siku 30 tunatoa notisi ya siku nyingine
30 za kutumia nguvu, kwahiyo kuanzia sasa hivi anzeni kujipanga wenyewe na
kuondoka wakati Halmashauri ikifanya tathmini ya maeneo ya vijiji ambavyo ni
halali ya kuwagawia kwa wale watakaopenda kupewa maeneo huko", alisisitiza
Dk. Kigwangalla.
Alisema
sheria za uhifadhi haziruhusu mtu yeyote kuingia ndani ya maeneo ya hifadhi na
kuendesha shughuli za kibinadamu na kwamba kufanya hivyo ni kudharau Sheria na
Malmlaka zilizopo.
Alisema
kwa upande wa wananchi wa kijiji cha Handa ambacho kilianzishwa kimakosa ndani
ya pori hilo wataendelea kubaki mpaka pale wizara yake kwa kushirikiana na
Wizara ya Tamisemi na Ardhi zitakapoamua hatma yao ikiwemo ama kulipwa fidia
kupisha eneo hilo au waendelee kubaki na mipaka ya hifadhi isogezwe.
Katika
hatua nyingine, Dk. Kigwangalla ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori
Tanzania TAWA kujenga miundombinu ya kuvuta maji kutoka katika chemchem iliyopo
ndani ya hifadhi hiyo na kuyasogeza kwenye makazi ya wananchi ili kulinda chanzo
hicho kwa kuzuia uharibifu unaofanywa na wananchi wanaofuata huduma katika eneo
hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana, alipotembelea kijiji hicho kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia akizungumza katika mkutano huo katika kijiji cha Handa wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...