Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
NAIBU Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile amesema hairuhusiwi katika duka la dawa kuwa na dirisha la ushauri kwani huo si utaratibu huku ikielezea sababu zinazosababisha usugu wa dawa.
Dk.Faustine Ndugulile amesema hayo jana katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Famasi yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Akizungumzia maduka ya dawa kuwa na dirisha kwa ajili ya kutoa ushauri, Dk.Ndugulile amesema kisheria hairuhusiwi kwani kuna mgawawanyo wa majukumu.
"Kuna baadhi ya maduka ya kuuza dawa wameweke na madirisha kwa ajili ya kutoa ushauri.Hairuhusiwi na hivyo baraza la famasi linatakiwa kusimamia hili kwa kuhakikisha hakuna duka la dawa ambalo limeweka dirisha la ushauri,"amesema Dk.Ndugulile.
Akizungumzia usugu wa dawa kwa mtumiaji, Dk.Ndugulile amefafanua zipo sababu nyingi ikiwamo ya matumizi ya dawa yasiyo sahihi na ulaji holela wa dawa.Amefafanua mbali ya kuwapo kwa sababu hizo kuna tafiti ambayo imebaini kuna vimelea ambavyo ni sugu wa hali ya juu kwa dawa zote zilizopo duniani.
Wakati huohuo Dk.Ndugulile ameliezea baraza la Famasi kuwa anao ushahidi wa baadhi ya watalaam wa famasi si waaminifu kwani wamekuwa wakiiba dawa na hivyo hao wachache kuharibu sifa ya famasi.
Ameliomba baraza la famasi kuhakikisha wanachukua hatua dhidi ya wanaokiuka sheria za famasi kwani kukaa kimya kunatoa nafasi ya baadhi yao kukika sheria zilizopo, hivyo wafuatilie.Hivyo amesema wenye tabia hiyo ya kuiba dawa waache mara moja kwani Wizara yao inafuatilia huku akielezea kwa sasa hakuna tatizo la uhaba wa dawa kwani zipo za kutosha.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi zawadi baadhi ya wadau wa Famasi kwa mchango wao katika sekta hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi zawadi baadhi ya wadau wa Famasi kwa mchango wao katika sekta hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akionesha juu Bango Kitita la famasia baada ya kulizindua wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam. Kulia ni Msajili wa Baraza la Famasia Bi. Elizabeth Shekirego Kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhamed Bakari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...