Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Aliyekuwa Mshambuliaji wa timu ya Mbao FC msimu uliopita, Habib Kyombo leo amesaini mkataba wa miaka mitatu na Singida United.
Kyombo
ambaye ameitumikia Mbao FC kwa mwaka mmoja na nusu alifanikiwa kufunga
mabao 16 kwenye mashindano yote aliyocheza akiwa na timu hiyo.
Ujumbe
wa shukrani aliondika kupitia mtandao, amesema anawashukuru Mbao FC na
mashabiki wake, kwa kusema kuwa tangu amevaa Jezi ya timu hiyo walimpa
sapoti yakutosha.
Bila
kusahau amemshukuru, Aliyekuwa Kocha wa timu ya Mbao, Ettiene
Ndayirajige kwa imani yake nakuonyesha kumuamini katika nafasi ya
ushambuliaji ambao imesaidia kumsogeza karibu na ndoto zake.
Amesema
hatosahau na itabaki kumbukumbu kwake baada yakuisaidia timu hiyo
kufika Fanali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation
Cup) msimu uliopita ambapo walipoteza kwa kichapo cha bao 2-1 mbele ya
Simba SC.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...